Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba, wilayani Kondoa, wakati wa ziara
ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa
chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya
CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
ziara yake hiyo aliyoambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye ilikuwa ya mafanikio makubwa, kwani msafara wake umetembelelea
Wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi kwa kuzunguka jumla ya Km, 2289.
Akizungumza
katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo mjini Kondoa, Nape alisema
kuwa katika mkoa huo tayari wamefanya mikutano 91, ambapo 82 ya hadhara
na 9 ya ndani. Pia wamekagua jumla ya miradi 73 ikiwemo 62 ya maendeleo
na 11 ya chama,Nape akaongeza kuwa katika ziara hiyo imefanikiwa
kuongeza wanachama wapya wapatao 8245
Kesho
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape Nnauye wanaanza ziara ya kikazi
katika Mkoa wa Arusha, ambapo wataanzia Jimbo la Monduli linaloongozwa
na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Kondoa, Zabein Mhita akijiandaa kupiga magoti ikiwa ni
ishara ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kusaidia kutatua
tatizo la maji katika Mji wa Kondoa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa sabasaba,jioni ya leo wilayani Kondoa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika
Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, ambapo amemshauri Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya
Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukka pamoja kupata suluhisho la
migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa
Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi
ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
Ndugu Kinana akihutubia katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa mgolole ikiwa ni heshima kubwa ya wazee wa kijiji cha Changaa,wilaya ya Kondoa
Mkuu
mpya wa Wilaya ya Kondoa, Shaban Kisu akijitambulisha wakati wa mkutano
wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Kisu ambaye alikuwa
mtangazaji wa TBC ameteuliwa hivi karibuni na Rais kushika wadhifa huo.
Mkuu
mpya wa Mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa akijitambulisha wakati wa
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Mh.Galawa
alikuwa mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mbunge
wa Jimbo la Kondoa Zabein Mhita akielezea utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Changaa.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,Kinana amemshauri
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa
minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata
suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na
askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa
risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano
huo.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akionyesha maganda ya risasi yaliyotumiwa na askari Nyama Pori na kuwajeruhi wananchi
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,
Wananchi wa Kata ya Kwadelo wakinyoonsha mikono juu kukikubali Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko vyama vingine vya siasa.
Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Kwadero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana haonekani pichani akishiri kuweka jiwe la msingi kwa ofisi ya CCM wilayani Kondoa.
Moja ya Jengo la Kituo cha Kilimo ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia alikagua.




















