Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate, (kulia), na
Meneja Miundombinu ya IT wa Mfuko huo, Gilbert W. Chawe, (katikati),
wakimsikiliza afisa mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Rehema Kabongo, wakati wa ziara ya Maafisa
kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mafao ya Uzeeni, nchini Kenya, (RBA), kwenye
makao makuu ya PPF barabara ya Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam.
Maafisa
toka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tanzania,
(SSRA) na wenzao kutoka Kenya (RBA), wakisikiliza mada zilizokuwa
zikitolewa na mameneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati maafisa hao
walipotembelea makao makuu ya PPF kwa nia ya kujifunza shughuli za
uhifadhi wa mafao na pensheni.
Maafisa
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifuatilia kwa makini wakati wa mkutano
baina ya viongozi wa PPF na maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya
Usimamizi wa Mafao Ya Uzeeni kutoka Kenya, (RBA), walioongozwa na
wenyeji wao SSRA kwenye ziara yao ya kujifunza walioifanya makao makuu
ya Mfuko huo barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam.
Afisa
mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao ya Uzeeni nchini Kenya,
(RBA), Timoth Chege, (kushoto), akiuliza swali wakati wa mazungumzo
baina ya maafisa hao kutoka Kenya walioongozwa na maafisa kutoka Mamlaka
ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, nchini SSRA na uongozi wa
Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa ziara ya maafisa hao kwenye makao
makuu ya PPF jijini Dar es Salaam, Kulia ni Rehema Kabongo kutoka SSRA.
Meneja
wa Huduma kwa Wanachama, wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Godfrey Mollel,
(wanne kushoto), akitoa maelezo kwa maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Mafao ya Uzeeni nchini Kenya, (RBA), na wale wa SSRA, wakiangalia jinsi
mfumo wa kuhudumia malipo kwa wastaafu unavyofanya kazi wakati
walipotembelea makao makuu ya PPF jijini Dar es Salaam kwa nia ya
kujifunza.
Meneja
wa Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Godfrey Mollel,
(wa pili kushoto), akitoa maelezo jinsi idara yake inavyohudumia wateja
kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya kupitia njia ya simu, wakati wa ziara
ya Maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao wa Wastaafu
nchini Kenya (RBA), wealiofuatana na wenyeji wao wa Tanzania SSRA, wa
pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Vupe Ligate, na wa kwanza
kushoto ni afisa kutoka SSRA Rehema Kabongo.
Meneja
wa Miundombinu ya IT wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gilbert W Chawe,
(kulia), akitoa maelezo wakati ujumbe huo wa RBA kutoka Kenya,
ulipotembelea chumba cha wataalamu wa compyuta wa PPF.








