KAULI ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kuwa kiasi cha shilingi milioni 10
alizotoa haraka kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow alizowekewa na
mfanyabiashara James Rugemalila zilikuwa ni za mboga, zimewakera mastaa
kiasi cha kumshambulia na kumuita mwenye dharau iliyopitiliza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar kwa njia ya simu, walisema fedha hizo ni nyingi ambazo zingeweza kuwasaidia wagonjwa mbalimbali, uchimbaji wa visima, kusaidia elimu, chakula kwa familia zisizojiweza na makundi mengi yenye uhitaji.
Walisema kauli hiyo inaonyesha jeuri waliyonayo watumishi wa umma, ambao hupata fedha nyingi kwa njia zisizo halali kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru. Mastaa hao ni pamoja na Baby Madaha, Nisha, Thea, Isabela, Tiko na Amanda Poshi.