Wakazi
wa Segerea wakiwa katika foleni kwaajili ya kuendelea na zoezi la
kupiga kura katika kituo cha Magereza Segerea muda huu huku hali ya
usalama ikiwa shwari kabisa
Foleni
ikiwa bado ndefu huku mwamko ukiwa mkubwa kwa rika zote kuanzia vijana
na wakina mama na baba zoezi linaendelea vizuri mpaka sasa
Blogger
Josephat Lukaza akiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo changu
cha Magereza segerea kwaajili ya kupiga kura kumchagua kiongozi
atakayenifaa
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Wakazi
wa Segerea ambao wamjiandikisha katika kituo cha Segerea Magereza
wakiwa wamejitokeza kwa wingi muda huu katika kituo hiko kwaajili ya
kushiriki zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi mbalimbali kuanzia
Rais, wabunge na Madiwani. Hali ni shwari hakuna vurugu wala viashiria
vyovyote vile vya vurugu japokuwa kuna changamoto za hapa na pale ambapo
mkazi mmoja ameambiwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa hawezi kupiga kura
kutokana na namba ya Kitambulisho chake cha kupigia Kura kutofautiana
tarakimu moja tu na Namba ya kitambulisho iliyoandikwa katika karatasi
la majina ya kuhakiki. Mkazi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe
amesema kuwa anasubiri Mkuu wa kituo cha Uchaguzi Segerea Magereza
kuweza kuongea nae na Kutatua swala hilo endapo ataruhusiwa basi atapiga
kura na asiporuhusiwa basi hatopiga kura
Wakazi wa Segerea wakiwa kwenye foleni kusubiri kupiga kura
Baadhi ya wakazi wa segerea wakiwa katika foleni tayari kwa kupiga kura.Picha Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Endelea kuwa nasi hapa tutakuletea kila kinachojiri kwenye vituo vilivyo karibu yetu
0 comments:
Post a Comment