Mtakatifu
Yuda Tadei,/ Mtume Mtakatifu,/ mtumishi mwaminifu na rafiki wa Yesu./
Jina la yule msaliti aliyemwuza Yesu/ limewafanya wengi wakusahau./
Walakini Kanisa zima linakuheshimu/ na kukuomba kama Msaidizi katika
mashaka makubwa,/ na katika mambo yasiyo na matumaini tena./
Uniombee
mimi mnyonge./ Ninaomba utumie uwezo ule uliojaliwa/ wa kuleta upesi
msaada kwa watu walioukosa./ Unisaidie sasa katika mahitaji yangu,/ ili
nipate kitulizo na msaada wa mbinguni/ katika lazima zangu,/ masumbuko
na mateso,/ hasa/ (taja shida yako)./ Pia ili niweze kumsifu Mungu nawe
na wateule wote milele./
Mtakatifu Yuda Tadei,/ utuombee,/ na uwaombee watu wote wanaokuheshimu na kukuomba msaada./
Moyo Mtakatifu wa Yesu,/ Rafiki mpenzi wa Yuda Tadei,/ nakutumainia./
(Mwisho Sali: Baba yetu (x3), Salamu Maria (x3) na Atukuzwe(x3).
0 comments:
Post a Comment