Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi akizungumza
na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es
Salaam ambapo ameruhusu upimaji wa vipande vya ardhi na utoaji wa
hatimiliki za ardhi uliokuwa umezuiliwa tangu kutangazwa kwa mradi huo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki
akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji
mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi akisisitiza
jambo wakati wa mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji
mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Bw. Meck Sadiki. Sehemu ya wadau hao ni pamoja na viongozi wa
taasisi za Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), madhehebu
mbalimbali ya dini na taasisi za elimu na ulinzi na huduma mbalimbali
zilizopo katika eneo hilo la Kigamboni.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Sellasie Mayunga akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi pamoja na
Naibu wake Mhe. Angellah Kairuki wakimsikiliza mmoja wa wadau Bw.
Nyaronyo Kicheere nje ya ukumbi wa mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi Sophia Mjema akizungumza wakati wa mkutano huo.