Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifanya
mahojiano
na Ephraim Kibonde wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba cha Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Michael
Chilongani wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwafafanulia jambo wageni
waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni
kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za
makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Mkurugenzi
wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwafafanulia
jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria
jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba
hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah
akibadilishana mawazo na wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za
makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar
es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Sophia
Mwema wa Shirika la Nyumba la Taifa akibadilishana mawazo na mmojawapo
wa wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana
jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo
za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu
Mbunge wa
Lushoto, Henry Shekifu akijadiliana jambo na mwenzake kwenye uzinduzi
wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa
rasmi Jumatatu.
Gibson
Mwaigomole wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwafafanulia jambo wageni
waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni
kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za
makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
Baadhi ya
wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za
Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu
David
Shambwe, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara, David Shambwe akishuhudia
namna shughuli hiyo inavyoendelea. Picha zaidi za tukio hili tutawaletea
......................................................................................................................
TAARIFA YA UUZWAJI WA NYUMBA ZA VICTORIA PLACE, DAR ES SALAAM
Kwa
mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Ijumaa, 6,
Machi, 2015) limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa
Victoria, jijini Dar es Salaam. Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha
zaidi ya Sh 11 bilioni mpaka utakapomalizika.
Mradi
huu upo Victoria Kijitonyama, takribani kilomita 7 kutoka Jijini Kati,
una nyumba 127 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo pacha ya ghorofa 13.
Mradi huu uko sehemu yenye huduma zote muhimu za kijamii jijini Dar es
Salaam zikiwamo za kiafya, shule, maduka, na masoko. Mbali na huduma
katika ujirani, mradi wenyewe utakuwa na maeneo ya biashara katika
ghorofa ya chini (ground floor) na ghorofa ya kwanza, ambapo tunatarajia
kuwepo na huduma nyingine za kijamii kama vile “Supermarkets”, Migahawa
n.k
Kadhalika,
Mradi huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani
umejikamilisha kwa huduma za wakazi,kwa kuwa na maeneo mawili ya ,
mazoezi (gym), mabwawa ya kuogelea mawili (swimming pools) na eneo la
watoto kuchezea.Zaidi ni kwamba, nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili ya
usalama watumiaji na kuna maegesho ya magari ya kutosha.
Mradi
una nyumba 127 tu zinazouzwa, zenye ukubwa tofauti, idadi ya vyumba
tofauti na bei tofauti. Nyumba hizi zina vyumba kuanzia viwili hadi
vinne, na bei zake zinaanzia Tshs165,150,000/= hadi 306,445,000/= kabla ya kodi ya Ongezeko la thamani(VAT). Ukubwa
wa nyumba unaanzia mita za mraba 90 hadi 167. Mbali na vyumba vya
kulala, kila nyumba ina jiko kubwa la kisasa, choo cha pamoja na eneo la
kufulia na kuanikia nguo.
Sifa
za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka, sehemu
iliyotengwa maalum kwaajili ya kufanyia mazoezi, bwawa la kuogelea na
eneo kubwa la ziada la maegesho ya magari.
Nyumba
hizi ni Bora na za Kisasa. Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania
wote walio nchini na walio nje ya nchi, wafanye mawasiliano na makao
makuu ya shirika, ofisi zetu za mikoa, au kupitia barua pepe na
kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato
ulio wazi wa manunuzi.