"Screen
shot" ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog
uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni
mwa mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia
mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na
mengine mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo
wanayoyatumia vibaya.
Kupitia
BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea
taarifa ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini
kwa sasa hilo halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha
blog imetoa mwanya kwa wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni
mwa mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu
yoyote anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email,
watu wanaoziendesha BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za
uongo, upotoshaji, habari zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na
habari ambazosi za kweli.
Tunaamini
wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri
tu licha ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’
habari nzuri na zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za
kuelimisha jamii, kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea
wengi sana kiasi cha hata kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni
binafsi ya kibiashara, Serikali na watu wengine, lakini shida ni kwenye
hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao kazi yao kukopi na ku-paste
habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye blog zao wengine
habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha kichwa cha
‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni haki?,
tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama
kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), ( https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke
huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao
waliifungua ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa
inabadilika kuwa wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae
wakawa wanaweka picha za viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho
wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si
mambo.
Hivyo
ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume
na maadili ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha
watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao
huu unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni
yao juu ya kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika
habari hii ni pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja
ya habari kwenye miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo
Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko
mochwari kwani amefariki huyo?” wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa
inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na habari kwenye hizo blog
uchwara.
Wadau
waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi:
“hahaha.... hili ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO
bongo kujifanya blogger and a self-appointed journalist... UJINGA mtupu,
huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu chefu... full of
attention-seeking sensationalism... utakuta heading: HATARI, Vilio na
majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog
zao.” Alieleza Mahundi.
Hata
hivyo wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari
na sheria ya ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
Modewji blog
tunaamini pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger
Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo
ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi
bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo, mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.