Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Luteni Mstaafu Abdallah
Kihato (wa pili kulia), akipokea Hundi ya Sh. Milioni 56 kutoka kwa
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kusini, Bw.
Victor Kavishe (wa pili kushoto) kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji
katika Kijiji cha Magoza, kilichoko Kata ya Kiparang'anda. Kushoto ni
Meneja Mahusiano wa TBL, Bi. Emma Urio na Diwani wa Kata hiyo, Bi. KAru
Karapina.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Kusini, Bw.
Victor Kavishe (wa pili kushoto, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,
mkoani Pwani, Luteni Mstaafu Abdallah Kihato, Hundi ya Sh. Milioni 56
zilizotolewa na Kampuni hiyo kwa ajili ya kusaidia mradi wa Maji katika
Kijiji cha Magoza, kilichoko Kata ya Kiparang'anda. Kushoto ni Mkuu wa
Mahusiano TBL,
Bi. Emma Urio na Diwani wa Kata hiyo, Bi. Karu Karavina. (Na Mpigapicha Wetu)
Akionesha Hundi aliyopewa na TBL
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, iliyoko Mkuranga, mkoani Pwani, Bi.
Karu Karavina akiishuikuru Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), baada kampuni
hiyo kutoa Hundi ya Sh. Milioni 56 za mradi wa maji katika kijiji cha
Magoza.. Walioketi kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Mstaafu
Abdallah Kihato na Meneja Uhusiano TBL, Emma Urio.
Afisa Uhusiano wa TBL. Bi. Doris Malulu akiungana na kinamama wa Kijiji
cha Magoza kuomba dua ili maji yapatikane katika kijiji hicho.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Urio
akizungumza na wananchi wa Magoza, kabla ya kampuni hiyo kukabidhi sh.
milioni 56 za mradi wa maji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya GCL, Bw. Gerald Mosha (kushoto) akiomba dua
pamoja na wananchi wa Kijiji cha Magoza kwa ajili ya kufanikisha mradi
wa maji.
Diwani
wa Kata ya Kiparang'anda Bi. Karu Karapina akikabidhi zawadi mbalimbali
zilizotolewa na wananchi wa Magoza kwa ajili ya TBL.