Kampuni
ya Simu Tanzania(TTCL) yakabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa
mafuriko Kahama. Msaada uliotolewa ni pamoja na mchele kilo 740, unga
kilo 600, maharage kilo 300 na mafuta ya kupikia lita 260.
Msaada
huo umekabidhiwa na Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru kwa
niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt.
Kamugisha Kazaura.
Akizungumza
baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Bw. Peter Kuguru alisema
TTCL inawapa pole sana wahanga wa tukio hilo na kwamba TTCL imepokea kwa
huzuni kubwa tukio hilo na kuwataka Watanzania kuwaombea waliopatwa na
janga hilo wapate faraja na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waliopoteza
maisha awapumzishe mahali pema peponi.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.Benson Mpesya akizungumza baada ya kupokea
msaada huo, aliishukuru TTCL kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa
mvua hiyo na kuongeza kuwa TTCL wamekuwa na moyo wa huruma kwa wahanga
hao huku akiahidi kuwa misaada inayotolewa na watu wenye mapenzi mema
itatumika kwa wahanga wa tukio hilo na si vinginevyo na atakuwa mkali
kwa hilo.
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (Kushoto) akipokea msaada kutoka kwa
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru(Kulia).
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru (Kulia) akikabidhi msaada kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (Kushoto).
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akitoa neno la shukhurani baada ya
TTCL kukabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama.
Wananchi
wakiongozwa na Kundi la Scout wakishusha msaada wa chakula kwa ajili ya
wahanga wa mafuriko yaliyotokea wilayani Kahama hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza na Wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Shinyanga .







