WANANCHI WAONYESHA MWITIKO MKUBWA WA ACCESSBANK WAKALA
Mr Muganyizi akiwa na Mkurugenzi wa AccessBank mkoa wa mbeya aliye mtembelea leo ofisini kwake ndugu Emanuel Venance
Siku zote ukitembelea
ofisi za Marketing huwezi toka kapa lazima upate zawadi mbili tatu
pichani ni Joshua Mutunga akiwa amezawadiwa zawadi safi kabisa akiwa na
Mr Andrea Ottinna katika tabasamu la aina yake. .
Afisa mkuu wa masoko Mr
muganyizi akifurahia jambo na Mr Elibariki Robert wakiwa katika
mohojiano leo ofisini na Blogu Ya Wananchi . Alisema tangu AccessBank
ilipoanzisha mfumo wa utoaji wa huduma za kibenki kupitia mawakala
mitaani ,wateja wamekuwa wakimiminika kwa wingi kwa mawakala walio
teuliwa nawamekuwa wakifurahia huduma zitolewazo ambazo wateja hao
wameipongeza benki kwa kusogeza huduma zake karibu nao. Nae bwana Muganyizi
amewaasa wananchi kujitokeza na kutembelea mawakala hao kwa ajili ya
kufungua akaunti na kuweka na kutoa hela pamoja na kufanya miamala hata
baada ya muda sa kawaida na matawi ya banki.