KATI
ya vitu vinavyochukua nafasi kubwa sana katika maisha ya wanadamu,
wakivizungumza kila mara na hata kuomba ushauri, basi ni vile
vinavyohusu mapenzi.
Nimekuwa nikiandika mambo haya ya uhusiano na maisha, lakini asilimia kubwa ya ushauri ninaoombwa kutoka kwa watu mbalimbali ni juu ya kitu gani wafanye ili nyenendo zao za kimapenzi ziende sawa. Msichana ataomba ushauri juu ya nini afanye ili mvulana wake ampende na kijana naye hali kadhalika, atalia juu ya mwandani wake kutoonyesha kwa kiwango kikubwa kuhusu mapenzi yake.
Ni kutokana na sababu hizo, ndiyo maana mapenzi yamekuwa yakiongoza kati ya majanga yanayowapata wanandoa na walio katika uhusiano, kwa sababu kila mmoja anataka kuiridhisha nafsi yake juu ya mashaka yoyote aliyonayo kuhusu mwenzake.
Wapo baadhi ya watu wanaopenda sana uhusiano wao, kiasi kwamba wapo tayari kwa lolote ili mradi kuhakikisha kwamba mambo hayaharibiki. Wanaweza kukubali kulala nje huku wakipigwa na mvua, lakini unapowaambia kuhusu kuondoka kwenye ndoa zao hawawezi kukuelewa.
Vivyo hivyo pia, wengine wako tayari kuua, ili mradi kuhakikisha mwenza wake haondoki katika himaya yake. Na bahati mbaya, wapo pia wale ambao wanakubali kuumia ndani ya mioyo yao kwa muda wote wa maisha yao, kwa sababu wanaamini kusema kwao au kuamua lolote, ni kusambaratisha mapenzi yao.
Tatizo linakuja pale kila mmoja anapojiona mwenye haki ya kuwa mwamuzi wa suala lolote linalohusu ndoa au uhusiano. Hili ni kosa kubwa kwa sababu ndoa ni mkataba wa hiyari baina ya watu wawili. Hakuna aliye juu kuliko mwenzake, vinginevyo labda iwe ndoa ya mkeka, ya kulazimishwa au ya kufuata maslahi.
Inapotokea hivyo, ni wazi kuwa ndoa au uhusiano huu upo hatarini na hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kuinusuru. Lakini njia bora na salama zaidi ya kuinusuru ndoa au uhusiano wako ni kwa mhusika mwenyewe, yaani wewe, kukubali kujishusha ili kumaliza tatizo lolote linalotokea katika uhusiano huo.
Wote tunajua, mizozo katika uhusiano au ndoa ni jambo lisiloepukika; maana yangu hapa ni kwamba utakuwa ni mwongo, kama utatuambia kuwa hujawahi kupishana lugha na mwenzako wakati wa uhusiano wenu. Hili ni jambo la kawaida kwa sababu kuishi na mtu kila siku kuna mambo mengi.
Hata hivyo, tunajua kuwa uwezo wa kuthibiti tatizo ndani ya ndoa linawezekana na inakuwa rahisi zaidi kama kila wakati wa kujadili tofauti zenu, kila mmoja anakuwa tayari kujishusha. Unakuwa tayari kusikiliza hoja za mwenzako kwa umakini na inapokuwa zamu yako kujibu, basi nawe unazungumza kwa sauti ya chini, ya uelewa na yenye kuonesha dhati ya kulimaliza jambo vizuri.
Siku zote familia zetu zimekuwa katika hatari ya mizozo kutokana na kila mmoja kudhani kwamba kwa vile yeye ni mume, basi anatakiwa ndiye awe mtu wa mwisho katika uamuzi wowote. Hapana, mtu wa mwisho anapaswa kuwa yule mwenye hoja zinazokubalika kwa pande zote mbili.
Au mwanamke asitake kumpanda kichwani mumewe kwa sababu tu ni mzuri wa sura na umbo, eti ‘akizinguliwa’ atasepa. Hapana, kama unadhani wewe ni mzuri, usingekubali kuolewa au kushiriki uhusiano na uliyenaye.
Msisitizo wangu kwa mara nyingine ni uleule, kama kweli uko tayari kuinusuru ndoa yako katika kipindi kigumu cha machafuko, basi wewe uwe wa kwanza kujishusha kwenye majadiliano kwa sababu ni mwendawazimu tu, anayeweza kugomba wakati mwenzake akiongea kwa taratibu.