Jerry MuroMsemaji wa Timu ya Yanga |
Na Ripota wa Globu ya Jamii
Uongozi
wa Klabu ya Yanga umeishukia bodi ya Ligi kwa kile walichodai kuwa
wamechakachua kanuni kwa kuiruhusu Timu ya Simba kumtumia mchezaji
Ibrahimu Hajibu na kuitaka sheria zichukue mkondo wake huku wakigomea
mechi yao dhidi ya JKT Ruvu kusogezwa mbele.
Akizungumza
kwenye Makao Makuu ya Klabu hiyo leo, Msemaji wa Yanga Jerry Muro
amesema Bodi ya Ligi inayumbisha soka la Tanzania kwa kupindisha sheria
na kitendo walichofanya ni cha ubabaishaji na hawawezi kukikalia kimya.
"Umeshaona
wapi mtu anakosa, anakaa kujadili adhabu ya kupewa na mtoa adhabu,
Tanzania ni ya kwanza, halafu eti tunataka soka letu lisonge mbele,
litasonga mbele kwa stahili hii?"alisema kwa kuhoji.
Katika
barua ya Februari 27 iliyosainiwa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi
ya Ligi Fatuma Abdallah kwenda kwa katibu mkuu wa Simba Steven Ally
ilisema "rejea barua yako ya Februari 25 yenye kumbukumbu namba
SSC/29/2015/07/GS kwa niaba ya bodi ya ligi tumezingatia maombi ya timu
yako kutaka kwa mchezaji Ibrahimu Hajibu aruhusiwe kucheza mchezo wa
Simba dhidi ya Prisons na Simba dhidi ya Yanga na asicheze mchezo dhidi
ya Mtibwa Sugar.
"Kwa
kuzingatia mabadiliko ya katiba yaliyofanyika hivi karibuni, kwa barua
hii mchezaji yuko huru kucheza katika mchezo wa Simba na Yanga." ilisema
sehemu ya barua hiyo na nakala kutumwa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi,
Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Kamati ya waamuzi, msimamizi wa kituo Dar
es Salaam na Yanga.
Hata
hivyo Yanga walidai kuwa hawawezi kukubaliana na jambo hilo kwa kuwa
mabadiliko hayo ya katiba yalipendekezwa na bado hayajapata baraka ya
mkutano mkuu.
Kwa mujibu wa kanuni ya 37 (4) ya Ligi kinachozungumzia udhibiti kwa wachezaji inasema
klabu
zinatakiwa zitunze kumbukumbu za wachezaji wake waliyoonyeshwa kadi.
Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi 3 za njano au kadi nyekundu
itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na
magoli 3, halikadhalika mchezaji anatakiwa atunze kumbukumbu zake za
kadi na iwapo atacheza akiwa anatakiwa kutocheza kwa ajili ya kadi tatu
za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo.
Wakati
huo huo Yanga wamegomea mechi yao na JKT kusogezwa mbele na kudai kuwa
Machi 11 hawatapeleka timu uwanjani kwa kuwa watakuwa wakijiandaa na
mchezo wao na Plantiam ya Zimbabwe.
Katibu
mkuu wa Simba Steven Ally alipoulizwa kuhusiana na suala la kuandika
barua hiyo alisema "Ni kweli niliandika kama kupinga kanuni walitakiwa
kupinga kwenye kikao cha bodi ya Ligi sio sasa, kanuni ilishapitishwa,
na Yanga wanayo nakala tunashangaa sasa hivi wanavyopinga maamuzi ya TFF
na bodi ya Ligi basi waende Fifa."
Naye
Katibu mkuu wa Simba Steven Ally alipoulizwa kuhusiana na suala la
kuandika barua hiyo alisema "Ni kweli niliandika kama kupinga kanuni
walitakiwa kupinga kwenye kikao cha bodi ya Ligi sio sasa, kanuni
ilishapitishwa, na Yanga wanayo nakala tunashangaa sasa hivi
wanavyopinga maamuzi ya TFF na bodi ya Ligi basi waende Fifa."
"Tumejiandaa
mechi yetu na JKT tunacheza kesho (leo), na Jumapili tunacheza na
Simba, sasa bodi ya Ligi wanatuhujumu wanatupangiaje mechi tarehe 11
alafu tarehe 14 tucheze na Zimbabwe wanatutaka nini hao?" alihoji na
kuongeza.
"Mkakati
wetu ilikuwa tukimaliza mechi ya Jumapili akili yetu tunaelekeza kwa
Zimbabwe, nasema tena Machi 11 hatupeleki timu tupo tayari kushuka
daraja wakitaka waipeleke mbele zaidi tumalize na Zimbabwe."alisisitiza