https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA WILAYA YA NGORONGORO MKOANI ARUSHA.

     Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa pili kulia)akishiriki ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Sakala, wilayani Ngorongoro.Ndugu Kinana na ujumbe wake wako kati wa ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
     Komredi Kinana akisaidiana na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Telele kujenga vyumba vya madarasa ya kidato cha nne na cha tano katika Shule ya Sekondari Samunge, wilayani Ngorongoro.
     Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Wasso Ndugu Revocatus William Parapara. Awali ndugu Revocatus William Parapara alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ngorongoro kwa takribani miaka 15.
     Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa ngoma ya kabila la Watemi (Wasonjo) alipowasili katika Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, aliposhiriki ujenzi ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato cha nne na cha tano katika Shule ya Sekondari ya Samunge wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
     Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ngorongoro wakiwa katika mkutano na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mjini Loliondo
     Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza katika mkutano huo.
     Komredi Kinana akiingia kwenye mkutano wa hadhara katika Mji wa Waso, wilayani humo
     Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
     Komredi Kinana akipatiwa zawadi ya fimbo



    Kinana akihutubia katika mkutano huo.
     Komredi Kinana akiangalia ngoma wakati wa mapokezi katika mkutano wa hadhara mjini Wasso, wilayani Ngorongoro.
     Vijana wa jamii ya kimasai wakitumia simu kupiga picha wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika KJijiji cha Ngaresero, wilayani Ngorongoro.

     Komredi Kinana akivishwa pambo lenye shanga katika Kijiji cha Ngaresero

     Mmoja wa wanachama wapya wa CCM akipatiwa kadi na Komredi Kinana baada ya kujiunga katika Kijiji cha Ngaresero, wilayani Ngorongoro.


    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA WILAYA YA NGORONGORO MKOANI ARUSHA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top