Katika
ziara hiyo Wahariri hao walipata maelezo mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa TBL,Roberto Jarrin kuhusu hali ya kibiashara ya kampuni hiyo pamoja
na bidhaa zinazozalishwa kisha kutembelea mitambo ya kutengeneza Bia.
Meneja
wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari aliwaambia Wahariri Changamoto
ambazo Kiwanda hicho kinakabiliana nazo kuwa ni pamoja na umeme wa grid ya
taifa kuwa na nguvu ndogo ya kutokutosha kuendesha mitambo, ubovu wa
barabara ya kuingilia kiwandani pamoja na upatikanaji wa maji.
Akitoa
Shukrani kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa TEF, Absolom Kubanda,
aliishukuru Kampuni ya TBL kwa kuwathamini na kuwaalika katika ziara hiyo
na kuongeza kuwa watakuwa mabalozi wazuri kutangaza hali halisi waliyoiona
kiwandani hapo tofauti na maneno ya watu mitaani.
Alisema
watu wengi hudhani mazingira ambayo vinywaji vinatengenezwa hayafai jambo
ambalo sio la kweli kutokana na kujionea wenyewe mlolongo mzima tangu
uoshaji wa chupa hadi kinywaji kinavyojazwa kuwa katika hali ya usafi.
Kwa
upande wake Meneja uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi alisema
lengo la kuwaalika Wahariri wa Vyombo vya habari ni kudumisha uhusiano
baina ya TBL na Vyombo vya habari.
Aliongeza
kuwa lengo lingine ni kutoa mrejesho kwa jamii juu ya hali ya kibiashara
ilivyosasa na awali kupitia kwa Wahariri wa Vyombo vya habari ili iwe wazi
kwa kila mtu.
|