Stori
ambayo kwa sasa imechukua headlines kwa wingi ni ile ya tetemeko la
ardhi lililotokea huku Nepal na kuua maelfu ya watu karibu na milima ya
Evarest.
Idadi ya
watu ambao wamethibitishwa kuaga dunia wakati wa tetemeko hilo
lililotokea siku ya jumamosi iliyopita imeongezea na kufikia zaidi ya
watu 5000.
Serikali
ya nchi hiyo imesema zaidi ya watu 10,000 walijeruhiwa na kuongeza
kuwa imelemewa na kiwango cha janga hilo hivyo inahitaji msaada kutoka
Mataifa mengine.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Sushil Koirala
amesema Serikali yao imepokea maombi mengi ya misaada kutoka maeneo ya
mbali lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na uhaba wa
vifaa na waokoaji.
Waziri huyo amesema kuwa kuna mahitaji ya dharura yanayohitajika yakiwa ya mahema , chakula pamoja na maji.