JESHI LA ULINZI LA
WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo
: “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES
SALAAM,
28 Aprili, 2015.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe
: ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti
: www.tpdf.mil.tz
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Iddi Mbita
(mstaafu) kilichotokea tarehe 26 Aprili 2015,
Brigedia Jenerali Hashim Mbita
(mstaafu) alizaliwa tarehe 02 Novemba 1933 katika mtaa wa Songoro, Kata ya Gongoni,
Wilaya ya Tabora Mjini, katika Mkoa wa Tabora.
Alisoma shule ya Msingi ya Government Town Primary School Mkoani Tabora
kuanzia mwaka 1946 hadi 1949. Alijiunga na Government Secondary School Tabora
Mwaka 1950 hadi alipohitimu kidato cha sita Mwaka 1957. Mwaka 1960 alijiunga na
Chuo cha East African School of Co-operatives kilichopo Nchini Kenya.
Marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita baada ya
masomo yake alijiunga na JWTZ tarehe 01 Novemba, 1968 na kutunukiwa Kamisheni tarehe
26 Aprili, 1969. Alistaafu Utumishi Jeshini
kwa Heshima tarehe 31 Desemba 1992.
Katika utumishi
wake marehemu alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi msaidizi Mkoa wa Mwanza
mwaka 1958 hadi 1960, Afisa Habari Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1960 hadi 1962,
Afisa Habari Mkuu wa Serikali mwaka 1962 hadi 1965, Mwandishi wa Habari wa Rais
mwaka 1965 hadi 1967, Katibu mwenezi wa TANU Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1967 hadi 1968,
Mwalimu wa
Siasa Chuo cha Maafisa Monduli 1969 hadi 1970, Katibu Mtendaji wa OAU Kamati ya
Ukombozi mwaka 1972 hadi 1989 na Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe mwaka 2003 hadi
2006.
Marehemu Brigedia
Hashim Mbita ameacha mke na watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe
29 Aprili, 2015 kuanzia saa 1:30 hadi 5:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi
Lugalo na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa
10:00 jioini baada ya Sala ya adhuhuri.
MUNGU
AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA
JENERALI HASHIM IDDI MBITA (MSTAAFU)
AMINA
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi,
Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano
zaidi: 0783 – 309963