Afisa
masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa
chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti
inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo
jana. Airtel
Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora
zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu.
Meneja
masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili
waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya
uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya
Airtel kuzindua huduma yao ya intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi maalum
kwa wanafunzi wa chuo hicho jana.
Mshauri
wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea
na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata
intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
Wanafunzi 60,000 wa UDOM kufurahia Airtel WI-FI
• Pia Airtel yazinduzi mnara wa pili UDOM
Dodoma, Aprili 27, 2015,
kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa
kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye
chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma
ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa
wananfunzi kwa gharama nafuu.
UNI
WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma
kupata huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na
kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo
hii tunazindua Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa
bei nafuu kwa ajili ya wanafunzi na pia tumeongeza mnara wa pili wa
simu ambao tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua
uchumi wa nchi yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya ".
Tunafuraha
kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni
kwani spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao,
kupata habari mbalimbali za taaluma au kijamii kupitia mtandao wetu wa
Airtel "
Meneja
Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi
itakuwa inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa UDOM, kwa kutumia simu
zao za mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM
bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia.
Wanaweza
kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana masaa 24 , kwa kifurushi
cha siku , wiki, mwezi na kifurushi cha usiku mzima.
Fikiria! Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi 500 tu! Alisisitiza Bi, Muga
Kwa
upande wake mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM)
Bw, Dick Manongi alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel Tanzania kwa
ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni. Nina
hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea
wanafunzi urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa
nchini na hata nje ya nchi ".
Ningependa
kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza
ujuzi wao kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae.
Uzinduzi
wa Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya
Airtel Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint
Augustine (SAUT) jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia
vyoo vingine hapa nchini.