Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akipata
maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo la hifadhi lililoombwa kwa
ajili ya upanuzi wa manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya waziri wa
maliasili na utalii mkoani Iringa leo. (Picha zote na Loveness Bernard)
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akifafanua jambo katika
mkutano wa kutatua mgogoro kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka
hifadhi ya Ruaha (mbomipa). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi.
Na Loveness Bernard
SERIKAli imeagiza Jumuia zote za hifadhi za jamii (WMA) nchini
kutoingia mikataba na wawekezaji mpaka wanasheria wa wizara ya Maliasili na
Utalii kuiidhinisha.
Akizungumza mjini Iringa, Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kuwa jumuia hizo zimekuwa zikiingia mikataba
ambayo inasababisha wananchi kushindwa kunufaika na rasilimali za maliasili
zilizoko katika maeneo yao.
“Migogoro katika hizi jumuia imekuwa mingi karibu nchi nzima,
na kwa sasa nadhani imefika wakati kila mikataba lazima iangaliwe na wanasheria
katika wizara yangu ili tuweze kujua kama mikataba imekaa sawa”.
Nyalandu ambaye alikuwa mkoani Iringa kwa ajili ya kusikiliza
mgogoro wa WMA ya Mbomipa alisema kwamba kwa kipindi kirefu wananchi wa zaidi
ya vijiji 20 wilayani Iringa wameshindwa kunufaika na rasilimali hizo.
‘’Wananchi waishio katika vijiji zaidi ya 20 Iringa
hawajanufaika na rasilimali zilizoko katika hifadhi ya Ruaha kutokana na mfumo
ambao haujawa rahisi kwa watumiaji wa WMA wote nchini , wizara wameamua kurekebisha
ili waweze kuepuka migogoro kama hiyo na mikataba yote itakaguliwa na wizara’’
Aidha waziri huyo amekubali ombi la manispaa ya Iringa la
kuongeza eneo la iliyokuwa hifadhi ya taifa ya Kihesa kilolo kuwa eneo la
Manispaa hiyo kwa jili ya upanuzi wa mji wa Iringa.
Ombi hilo lilitolewa
na Manispaa ya Iringa ikiwa ni ombi la kutaka kubadilisha matumizi ya eneo hilo
lililokuwa hifadhi kuw amakazi ya watu kwa ajili ya upanuzi wa mji ombo
walilotoa kupitia kwa Waziri wa Ardhi Willia Lukuvi.