Jumamosi
iliyopita kuliripotiwa kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi katika
milima ya Everest, Nepal ambapo si mbali na makazi ya watu.
Katika tukio hilo magazeti yaliyotoka leo yana taarifa kwamba watu 2000 wamefariki pamoja na majeruhi zaidi ya watu 5000.
Mwndelezo
wa habari hiyo unasema mpaka sasa idadi ya watu waliofariki ni 3,600 na
huenda idadi ikaongezeka wakati wowote kutokana na hali za majeruhi
kuwa mbaya.
Idadi kubwa ya watu ambao wanaishi karibu na milima wako katika hali mbaya na kukosa makazi.
Athari
zilizojitokeza bado ni kubwa sana.. wapo watu wengi waliokosa makazi,
wengine waliamua kulala kwa zaidi ya siku mbili nje kabisa ya nyumba zao
huku wengine wakilala kwenye mahema yaliojengwa kwa mifuko ya plastiki.