Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani
Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani
Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii
CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya Uhamasishaji wananchi
kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya
Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati
ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata
Raymond.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KILWA)
Mkuu
wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akiangalia mashuka
150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa NHIF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa
wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga afya ya
jamii CHF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi,
Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi
Fortunata Raymond.
Mkuu
wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na
wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya
kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya jamii CHF.
Rehani
Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi
katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha
wananchi kujiunga na afya ya Jamii CHF.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF na madaktari
wakiandaa eneo la kuhudumia wananchi kwa upimaji wa afya wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.
Baadhi
ya wanahabari Othman Michuzi wa Michuzi Media na Fatuma kutoka Clouds
Lindi wakipata taswira mbalimbali katika uzinduzi huo.
Mkuu
wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na
baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni
ya kihamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya
kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF.
Mkuu
wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na
baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni
ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya
kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF na katikati ni Meneja wa NHIF mkoa
wa Lindi Bi Fortunata Raymond.
Rehani
Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi
wilaya ni Kilwa.
Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF.
Baadhi ya madaktari wakisubiri kuanza kutoa huduma katika uzinduzi huo.
Wananchi wakipima uzito.
Madaktari wakiwachunguza na kuwapima afya wananchi wa kijiji cha Njia Nne kata ya Tingi wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii Shoti na Faida wakiburudisha wananchi huku wananchi hao wakiendelea kupata huduma katika uzinduzi huo.
Wananchi wakiendelea kupima afya.
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF wakifurahia jambo wakati wa
uzinduzi huo kutoka kushoto ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na
Utafiti, Salvatory Okum Afisa Mfuko wa Afya ya Jamii, Fortunata Raymond
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi na Paul marenga Afisa Matekelezo na
Uendeshaji NHIF mkoa wa Lindi.
Mkuu
wa wilaya ya Kilwa, Bw Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma
wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa
zinapatikana muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.
Aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji
wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa
taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa
kata ya Tingi njia nne wilayani Kilwa.
Ulega
alisema serikali kupitia mifuko ya uchangiaji ya bima ya afya (NHIF) na
mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya
matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya
ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa
wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.
Awali,
mkurugenzi wa masoko na utafiti wa bima ya afya Rehani Athumani
alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa kampeni hiyo inayozinduliwa
itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya
halmashauri zilizohamasisha nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika
mwaka wa fedha wa 2014/15.
Amezitaja
halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji.
Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa
katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na
Itirima.
Naye
mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa mifuko ya afya
ya jamiii nchini (TNCHF) bibi Kidani Mhenga amewaahidi wananchi wa
mikoa ya Lindi ya Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua
changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia mfuko wa
afya wa jamii katika mikoa hiyo.
Ameomba
ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa
huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na
kusimamia huduma.
Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.