Wanajeshi wa Nigeria wakiimaklisha ulinzi dhidi ya Boko Haram nchini humo.
Jeshi
la Nigeria limesema limewaokoa wasichana 293 kutoka katika kambi ya
Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, Kaskazini-Mashariki mwa nchi
hiyo. Jeshi hilo limesema kuwa, wasichana hao waliokolewa siyo wale
waliotekwa na kundi hilo mwaka jana katika eneo la Chibok.
Akizungumza
na vyombo vya habari, msemaji wa Jeshi limeiambia limeongea na vyombo
vya habari kwamba, wanawake na wanawake na wasichana hao walikutwa
katika kambi nne tofauti Boko Haram ambapo silaha pia zimekamatwa,
ameongeza kuwa, Jeshi liliwapata mateka hao baada ya kuzivamia na
kuzishambulia kambi kisha kufanikiwa kuwaokoa.
"Ni
muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa
Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne
zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa
kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu." Alisema
kiongozi huyo.
Kwa
sasa Jeshi limezuiwa kutoa kuweka wazi majina ya mateka hao
waliookolewa kusisitiza kuwa wasichana hao siyo wale wanafunzi
waliotekwa katika mji wa Chibok mwaka jana.
Msemaji
wa Jeshi la Nigeria alisisitiza kwa kusema, "Tuko katika mchakato wa
kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini
kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana
mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok
waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea
kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote."
NA BBC