Na Saleh Ally
UNAWEZA kusema kila wakati una mfalme wake. Ndivyo ilivyo sasa katika Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) na LeBron James.James anayekipiga Cleveland amekuwa mchezaji anayeonyesha kiwango cha juu bila ya kuporomoka kwa kipindi kirefu.Wakati
anaondoka Miami Heat na kujiunga na Cleveland, wengi walitabiri ndiyo
mwisho wake James kwa kuwa aliondoka katika timu kubwa huku wakisema
ameamua kwenda kustaafu.
Lakini
mwenendo wake kwa sasa, unafanya waliofikiri anakwenda kustaafu
wabadili mawazo kwani amekuwa akiweka rekodi mpya kwa kuzivunja kadhaa
za zamani.
Baadhi ya rekodi ambazo amekuwa akivunja ni zile alizowahi kuziweka yeye mwenyewe.
James
amewahi kufunga pointi 61 katika mechi moja tu, hiyo ilikuwa ni wakati
Miami Heat iliposhindwa kwa pointi 124-107 dhidi ya Charlotte Bobcats.
Si
kwamba wengine hawajawahi kufunga, lakini ni nadra kutokea hivyo naye
amerudia mara kadhaa kufunga pointi 50 hadi 60 katika mchezo mmoja.
Amewahi
kufunga pointi 50 mara 10 katika michezo tofauti katika NBA. Amefunga
pointi hizo mara nane akiwa na Cleveland Cavaliers, mara mbili akiwa na
Heat.
James
ndiye mchezaji aliyefunga pointi tatu mara nyingi zaidi kama utahesabu
katika mechi 50 za NBA. Rekodi anayoishikilia pia ya kufunga pointi tatu
mara nane katika mitupo kumi anayolenga lango.
Angalau
Kobe Bryant ameonyesha naye ni mkali baada ya kuwa na rekodi ya kufunga
mikwaju ya pointi tatu mara nane katika mitupo 12.
Lakini James akaweka rekodi nyingine kali zaidi baada ya kufunga mitupo yote minane ya pointi tatu aliyotupa dhidi ya Bobcats.
Mkali huyo ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga pointi nyingi katika robo moja baada ya kuivunja aliyoikuta.
James alifunga pointi 25 katika robo moja, akawa amevunja rekodi yake aliyokuwa ameweka ya kufunga pointi 24 katika robo moja.
Kama hiyo haitoshi, James ameweza kuvunja rekodi ya muda wote ya pasi zilizozaa mabao au asisti katika NBA.
Anashikilia
rekodi ya msimu mmoja ya kutoa asisti nyingi zaidi. Msimu wa 2009-10
alitoa 651 akiwa na wastani wa 6.9 kwa mchezo mmoja.
Kwa msimu huu, tayari James ana wastani wa pointi 25.7 kwa mechi, asisti 7.3 na ribaundi 5.6.
Rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na mkali Scottie Pippen aliyeng’ara sana na Chicago Bulls enzi zake.
Wakati
akiitumikia Cleveland Cavaliers ikiitandika Detroit Pistons, James
alitoa pasi nzuri kwa mshambuliaji Kevin Love aliyepiga pointi tatu na
wao mwisho kushinda kwa 102-93.
Pippen
aliweka rekodi hiyo kwa karibu miaka 10 iliyopita na kuiacha wakati
anastaafu mwaka 2004 akiwa ametoa pasi zilizozaa pointi mara 6,135.
James
aliyefunga pointi 19 na kutoa asisti 11 katika mechi hiyo sasa
amefikisha asisti 6,142 na kubeba rekodi hiyo kwa wale wanaoendelea
kucheza.
Katika NBA wakiwemo waliostaafu, James sasa ndiyo kashika nafasi ya 27 nyuma ya Jerry West mwenye asisti 6,238.
Mkali
huyo ameendelea kufanya mengi licha ya kuwa amehama Heat, hali
inayodhihirisha kuwa uwezo binafsi na juhudi alizonazo zinaweza kubadili
mambo.