Kwa sababu unahitaji mawasiliano lazima
uwe na simu.. Kwa kuwa unahitaji mawasiliano bora na ya kisasa labda
ukajikuta unalazimika kuwa na smartphone.. Watu wengi wanapenda kutumia
smartphone kwa kuwa inarahisisha vingi.. Facebook, Twitter, Whatsapp unatumia
kiurahisi kabisa.
kiurahisi kabisa.
Baada ya hapo ikaja teknolojia ya kifaa
cha kutunzia umeme ili kama mtu ukiishiwa chaji kwenye simu yako na uko
mbali basi Power bank inasaidia simu yako kuendelea kuwa hewani kwa muda
mrefu zaidi.
GOOD NEWS kwako, huenda muda mfupi ujao usihitaji sana kutembea na Power bank yako.
Utafiti umefanyika Stanford University
California ambapo wamebuni betri aina nyingine ambayo hii unaambiwa
inajaa chaji kwa dakika moja tu.. ni rahisi zaidi na salama kuitumia
hii.
Wanasayansi wanasema hii betri itakuwa
salama zaidi kwa kuwa hailipuki kama ambavyo ziko betri nyingi
zinazotumiwa sasa hivi ambazo zimetengezwa kwa lithium.
Utaenjoy sana hii kwa sababu inajaa
chaji kwa haraka zaidi, japo betri hii inaisha kwa haraka ukilinganisha
na betri hizi za kawaida.. ila kama ukipata betri hii hautohitaji kukaa
muda mrefu kusubiri simu yako ijae chaji kwenye umeme.