Tumezoea kukutana na story za watu
kufumaniana majumbani.. kwenye nyumba za kulala wageni na kwingineko,
huyu bwana imemkuta Hospitali.. japo huwezi kuliita ni fumanizi lakini
jinsi ambavyo kagonganisha wanawake zake 17 ni ishu mtu wangu.
Yuan alipata
ajali ya gari China, akawa amelazwa Hospitali kuanzia March 24 2015..
sasa kama kawaida si kuna ndugu jamaa na marafiki wakapata taarifa
kwamba ndugu yao kapata ajali, wakawa wanakuja kumjulia hali.. mbaya
zaidi ikawa pale ambapo wasichana 17 ambao wote ana uhusiano nao
walifika kwa pamoja Hospitali tena bila kujuana.
Wang Fang ni mwanamke aliyezaa na Yuan
mtoto mmoja, amesema hakuwahi kuhisi kama mume wake ana uhusiano na
wanawake wengine, kwa sasa kajua hilo amekubali matokeo.. kasema hana
haja tena kumpenda mzazi mwenzake.
Mwanamke mwingine Xiao Li nae
alikuwa kwenye uhusiano na jamaa kwa zaidi ya miezi 18, alipata uchungu
kusikia mpenzi wake amepata ajali.. alipokutana na wasichana wengine
Hospitali wote wamekuja kumuona Yuan ilibidi uchungu wote umuishe.. ameona asahau kabisa suala la ndoa na mpenzi wake huyo.
Wanawake hao wamefungua group lao Facebook, eti kwa sasa wanajadili kuona jinsi ambavyo jamaa huyo amewachezea wote 17 kwa wakati mmoja na wasijue.