https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Unaweza kumiliki vigari vidogodogo kama Toyota IST na nyingine lakini zisifanane na hizi.

    IST 2Ni miaka kadhaa imepita ndipo nilipoamini gari ni mtu mwenyewe, yani wewe mmiliki ndio mwenye maamuzi kama utapenda gari lako liwe na swagg au muonekano wa kuvutia zaidi.

    Mara nyingi huwa tunayaacha magari yetu kama tulivyoyanunua na yanabaki yakawaida tu lakini kuna ambao hujiongeza alafu magari yao yanatofautiana na ya kwetu wakati aina ni ileile.
    IST 3Toyota IST ambazo zinatolewa na Airtel kupitia Yatosha Bundle ni gari nzuri kiukweli kuanzia kwenye mafuta, nafasi yake ndani ni kubwa pia na kwenye mishemishe zetu sisi tusio na kipato kikubwa kihivyo zinatuondolea gharama kubwa.
    IST 6Muonekano wa gari lako unaweza kubadilika na kuvutia kwa kuongeza vitu vidogovidogo tu kama kubadilisha Matairi na kuweka manene kiasi, rims kali, taa, tinted na vitu vingine kama muonekano wa mbele na wa nyuma.
    IST 8Magari makali yaliyokua pimped na yenye mvuto yapo Tanzania pia, ni vitu ambavyo vinawezekana hata ukiwa Dar es salaam kuna wachache wameweza kuyatengeneza kwa viwango vyao.
    IST 9Kama mapenzi yako yako kwenye vigari vidogovidogo kama hivi, kipi kimekuvutia hapa ?
    IST 10Magari yote hapo juu yanao muonekano tofauti na hili hapa chini ambalo halijafanyiwa mabadiliko yoyote toka kiwandani.
    IST 122
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Unaweza kumiliki vigari vidogodogo kama Toyota IST na nyingine lakini zisifanane na hizi. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top