Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama, leo anawaongoza watanzania katika kuadhimisha miaka 51 ya
kuzaliwa kwa Tanzania baada ya kuunganisha nchi mbili huru za Tanganyika
na Zanzibar.
Katika
muungano huu ambao leo hii tunausherehekea nikwamba Mwalimu Nyerere
alikuwa Rais wa kwanza na Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ),Sheikh Karume akawa makamu wa kwanza wa Rais.
Baada ya tukio
hilo sasa ambalo ni la kihistoria nchi ikaanza kutawaliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na Bunge la
Tanzania.
Nikukumbushe tu kwamba Mkataba wa muungano ulitiwa saini na aliyekuwa
Rais wa Tanganyika Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na aliyekuwa Rais wa
Zanzibar Hayati Sheikh Karume Aprili 22,mwaka 1964 mjini Zanzibar.
Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi waliuthibitisha mkataba huo
Aprili 26 na 27 mwaka 1964, viongozi wan chi hizo mbili walikutana
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kubadilishana hati ya
muungano.


