Soka
ndio mchezo wenye mashabiki wengi zaidi duniani, lakini watu huvutiwa
na mastaa wa soka na wengine hufuatilia hata maisha yao nje ya soka
yakoje, ndio maana mtu kama Beckham na familia yake wamekuwa wakifuatiliwa sana maisha yao licha ya kustaafu soka.
Hapa nimekuwekea list ya mastaa ambao hutazamwa zaidi na watu wengi katika maisha yao ya mahusiano ya kimapenzi.
1. David na Victoria Beckham
Unaambiwa hii ndiyo couple iliyokuwa na nguvu zaidi kwa upande wa wanasoka baada ya kufunga ndoa rasmi mwaka 1997, Beckham na mke wake Victoria wana watoto wanne ambao ni Brooklyn, Harper, Romeo na Cruz
2. Lionel Messi na Antonella Roccuzzo
Messi na mke wake ambao wote ni raia wa Argentina walianza mahusiano yao rasmi mwaka 2009, kwa sasa wana mtoto mmoja aitwaye Thiago aliyezaliwa Novemba 2012
3. Steven na Alex Gerrard
Hii pia ni miongoni mwa couple yenye nguvu kubwa katika soka la England na imekuwa ikitazamwa na watu wengi, wana watoto watatu Lilly, Lourdes na Lexie
4. Gerard Pique na Shakira
Camera za mapaparazzi zilikuwa karibu nao tangu walipoanza uhusiano wakati Shakira alipopata shavu la kufanya video ya wimbo wa ‘Waka Waka’ uliotumika wakati wa kombe la dunia mwaka 2010, wana watoto wawili, Sasha na Milan
5. Frank Lampard na Christine Bleakley
Walikutana wakati ambao Lampard alipoachana na mchumba wake ambaye wamezaa mtoto mmoja Elen, waliingia rasmi kwenye uhusiano mwaka 2011
6. Wesley Sneijder na Yolanthe
Sneijder na mkewe ambao ni raia wa Uholanzi walianza uhusiano mwaka 2009 na mwaka uliofuata waliamua kufunga ndoa
7. Iker Casillas na Sara Carbonero
Walianza uhusiano wao mwaka 2009, mpaka sasa wana mtoto mmoja anayeitwa Martin aliyezaliwa January 2010
8. Wyne Bridge na Frankie Sandford
Uhusiano wao ulianza mwaka 2010 wakati Bridge akiwa Manchester City, walifunga ndoa mwaka 2014 na sasa wana mtoto mmoja anaitwa Parker
9. Peter Crouch na Abbey Clancy
Crouch na Clancy wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu tangu mwaka 2006, wamejaliwa mtoto mmoja wa kike ambaye jina lake ni Sophia
10. Gareth Bale na Emma Rhys
Uhusiano
wao huenda ukawa kwenye rekodi kubwa zaidi, walianza urafiki tangu
wakiwa wadogo sana, safari ikafika hapa ukubwani sasa.. ni mume na mke,
wana mtoto mmoja ambaye anaitwa Alba Violet