 |
| Waziri
wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Simbarashe Mumbengegwi akifungua
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC) unaojadili Mkakati na Mwongozo wa kuelekea Maendeleo
ya Viwanda katika Kanda ya SADC. Mhe. Mumbengegwi amefungua mkutano huo
jijini Harare, Zimbabwe huku akiwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa ya
kifo cha Bregedia Jenereli Hashim Mbita ambaye alitoa mchango mkubwa
katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika. Mhe. Mumbengegwi
aliwaomba wajumbe wote wa mkutano kusimama ili kumuombea dua Bregedia
Hashim Mbita. |
 |
| Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Mb) wa katikati akiomba
dua kumkumbuka Brigedia Hashim Mbita. Kulia kwa Mhe, Kigoda ni Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) na kushoto kwake ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma Maalim (Mb) nao pia wakimuombea dua Brigedia Mbita. |
 |
| Meza kuu nayo ikimtakia kheri Brigedia Hashim Mbita. |
 |
| Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Stergomena Tax akitoa hotuba kwa Baraza la Mawaziri wa SADC. |
 |
| Waziri
wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Simbarashe Mumbengegwi akitoa hotuba
ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawziri wa SADC. |
 |
| Waziri
wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe akiangalia hotuba aliyekabidhiwa na Katibu
Mtendaji wa SADC, Bi. Tax mara baada ya kuwasilishwa na Katibu Mtendaji
huyo mbele ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC |
 |
| Kutoka
kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb); Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (Mb); Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) wakiwa na Mawaziri wa
nchi nyingine katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC. |
 |
| Picha ya pamoja ya Baraza la Mawaziri wa SADC. |
Matukio kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa SADC kuanza
 |
| Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (katikati), Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma Maalim (kulia) na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba
wakiwa katika kikao cha maandalizi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza
la Mawaziri wa SADC jijini Harare, Zimbabwe. |
 |
| Mhe. Kigoda akiendesha kikao hicho cha maandalizi. |
 |
| Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Musa Uledi wa kwanza kushoto
akitoa maelezo kwa Waheshimiwa Mawaziri juu ya agenda zitakazojadiliwa
katika Mkutano wa Mawaziri wa SADC. |
 |
| Makatibu
Wakuu wakiwa katika kikao cha maandalizi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu
Gamaha. |
 |
| Wataalamu mbalimbali wakiwa katika kikao cha maandalizi. |