Abiria
zaidi ya 50 wamenusurika leo baada ya basi walilokuwa wakisafiria
liitwalo Burudani kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta
maeneo ya Soni mkoani Tanga. Mashuhuda wamesema hii ajali imetokea baada
ya Lori la mafuta kukatika breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso.
Habari zinasema hakuna maafa yaliyoripotiwa hadi sasa ila watu kadhaa
wamepata majeraha na kukimbizwa hospitali.
Hii ni
ajali ya pili ya basi la abiria kutokea leo, ikufuatiwa na ile ya
asubuhi maeneo ya Msimba, Mikumi, jirani na milima ya Udzungwa ambapo
imeripotiwa kwamba watu 18 wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 10
kujeruhiwa baada ya lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na basi la
abiria na yote mawili kushika moto hapo hapo.