MKUU wa
Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akishuhudia wananchi wa
Kisiwa Panza wakizipanga bati baada ya kushushwa kwa ajili ya waathirika
wa maafa kisiwani huko.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
VIONGOZI
wa serikali ya Mkoa wa kusini Pemba, wakishuhudia gari ya aina isuzu
ikiteremsha bati zilizotolewa na Waziri wa Mwasiliani wa Tanzania Bara
kwa wananchi wa Kisiwa Panza waliopatwa na maafa ya nyumba zao hivi
karibuni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
WAZIRI
wa mawasiliano Sayansi na Tenkolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Mhe:Prifesa Makame Mnyaa Mbarawa, akizungumza na mkuu wa
Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla wakati wakielekea
kisiwa Panza kuwafariji wananchi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
MKUU wa
Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla akimpatia maelekezo Waziri
wa mawasiliano Sayansi na Tenkolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Mhe:Prifesa Makame Mnyaa Mbarawa, juu ya madras ya Qurania
iliyoanguka ukuta wake kutokana na upepo uliovuma kisiwa Panza na
kusababisha maafa kwa wananchi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
WAZIRI
wa mawasiliano Sayansi na Tenkolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Mhe:Prifesa Makame Mnyaa Mbarawa, akizungumza na wananchi wa
kisiwa Panza waliopatwa na maafa baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na
upepo hivi karibuni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
WAZIRI wa
mawasiliano Sayansi na Tenkolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Mhe:Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akiwakabidhi mabati wananchi
wa kisiwa Panza waliopatwa na maafa baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa
na upepomkali hivi karibuni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Item Reviewed: PROFESA MBARAWA AKABIDHI MABATI KWA WAATHIRIKA WA KISIWA PANZA
Rating: 5
Reviewed By: Unknown


