Tayari mashirika ya misaada ya kimataifa imeanza kupeleka misaada nchini humo.
Taarifa zinasema zaidi ya watu milioni moja na laki nne wanahitaji msaada wa haraka wa chakula.Tetemeko la ardhi lilipiga katika mji mkuu wa Nepal, Kathmandu siku ya jumamosi na kuharibu miundo mbinu mbalimbali zikiwemo nyumba kubomoka na kuwafukia mamia ya wananchi.
Zaidi ya watu 4,310 wamefariki dunia huku zaidi ya 8,000 wakijeruhiwa kufuatia tetemeko hilo.