Ni ukweli usio na shaka kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu wa zamani, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa ana dhamira ya kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha CCM.
Ni
ukweli usio na shaka pia kwamba ili afikie hatua ya kuwa mgombea urais
wa CCM ni lazima kwanza ashinde kwa kuruka na kuvuka “viunzi” na
“vigingi” vya Kamati ya Maadili, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano
Mkuu, ambavyo vyote hivyo ni vyombo vya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwa
mujibu wa hali ya hewa ya kisiasa katika nchi yetu kwa sasa, inaonekana
wenye “nia” ya kuiomba CCM ikubali kuwakilishwa na wao kwa nafasi ya
urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika, inshaa-Allah, mwishoni mwa
mwaka huu, wako wengi pengine wakaizidi idadi ya “wasaka urais” wa CCM
waliojitokeza mwaka 1995 na 2005.
Hapo tunaona kwamba “ushindani” ndani ya CCM juu ya ni nani haswa aiwakilishe, utakuwa mkali na mgumu mno.
Swali
ambalo ni muhimu na lazima litafutiwe majibu mapema ni kumtafakari kila
mgombea atakayeomba “ridhaa” ya CCM kuiwakilisha ni ipi faida ya
kuiwakilisha CCM na yapi madhara ya kutokuiwakilisha; hiyo ni tafakuri
ambayo ni muhimu kila mmoja wao kufanyiwa.
Kalamu
yangu kwa leo imeona iikumbushe CCM kufanya tafakuri hiyo kwa
Mheshimiwa Edward Lowassa kabla ya hao watarajiwa wengine. Ninapendekeza
tafakuri hiyo ianze kwa Mheshimiwa Lowassa kwa sababu:
(a) Ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye anaonekana kuwa na wapenzi na mashabiki wengi mpaka hivi sasa.
(b)
Ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye tayari ameshatamka kwamba katika
uongozi wake ataanzia pale ambapo Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete
atakapoishia (hiyo ni dalili kwamba “piga ua” atagombea tu).
(c) Ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye tayari amefuatwa na kushawishiwa na makundi kadhaa wa kadhaa.
(d) Ndiye mgombea mtarajiwa pekee ambaye wasifu wake na historia yake inamtofautisha na wagombea watarajiwa wengine.
Si
sahihi hata kidogo kumdharau au kuidharau jamii hiyo ya kitanzania
iliyojenga imani kwake, na ndipo nikaonelea nianze “uchokozi” mapema kwa
njia ya swali kwamba: Je, CCM imejiandaa na changamoto za kumkataa au
kumkubali Lowassa?
Katika
hali ya kawaida na kwa kutumia akili tu ya kuzaliwa, endapo Chama cha
Mapinduzi (CCM) kitamptisha Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa mgombea wake
wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao,
itapambana na changamoto kadhaa.
Lakini
hata kama CCM watakataa kuwakilishwa na Mheshimiwa Lowassa, bado pia
zitakuwepo changamoto kadhaa. Kwa muktadha huo, kumkubali Mheshimiwa
Lowassa ni tatizo, na hata kumkataa ni tatizo pia.
Mfano
wa Mheshimiwa Lowassa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni kama “tonge
tamu” la chakula cha moto ambalo ukilimeza utaungua na kulitema huwezi
kwa sababu ni tamu na unalihitaji.
Kazi
kubwa sana ambayo watapambana nayo viongozi wa CCM ni kuyapima madhara
na faida kwa kutumia kipimo huru kisichohusishwa na “shinikizo” lolote
lile.
Pamoja
na kwamba CCM ndio wanaowajibika na kazi ya kuufanya utafiti huo,
lakini kutokana na mazingira ya siasa za kitanzania kwa sasa tunaweza
kuyapima yale ya “juu juu” ambayo muonekano wake uko wazi. Halafu yale
ambayo ni ya “ndani zaidi’ yatatamkwa na wenyewe (makada na makomredi wa
CCM).
CCM
ikithubutu kufanya “mizengwe” na hila yoyote kumkataa Mheshimiwa
Lowassa kiasi kwamba, yeye Lowassa na wafuasi wake wakajiaminisha kwamba
“wameonewa”, basi CCM ijiandae kuzikabili changamoto zifuatazo:
(i)
Kwanza Mheshimiwa Lowassa, yeye mwenyewe haonekani kama atayapokea
matokeo hayo japo kwa shingo upande, bali upo uwezekano mkubwa wa
kukubali “maombi” ya kujiunga na chama pinzani chenye nguvu ili agombee
kupitia upinzani.
Na
hapo ni lazima CCM “ijiandae” kupambana na nguvu kubwa ya upinzani
ambayo itakuwa imeunganishwa na nguvu kutoka ndani ya CCM ya wale “CCM
Lowassa” ambao watakuwa wamekasirishwa sana kutokana na “kuenguliwa”
kipenzi chao, Mheshimiwa Edward Lowassa. Kwa mtazamo wa wafuasi hao,
“Lowassa kwanza, CCM baadae”.
Japokuwa
Wapinzani wamekuwa wakitamka hadharani mara kwa mara hawatohitaji
“makapi” ya CCM, lakini kamwe tusijidanganye kwamba Wapinzani watadharau
nguvu ya Mheshimiwa Lowassa katika kuwafanya Wapinzani wafungue ukurasa
mpya wa kuiondoa CCM madarakani kwa kutumia nguvu ya mwana CCM huyo
“mstaafu”.
Je, CCM wamejiandaa kukabiliana na nguvu hiyo ya Mheshimiwa Lowassa iliyounganishwa na nguvu ya vyama vya upinzani?
Je, CCM wamejiandaa kukabiliana na nguvu hiyo ya Mheshimiwa Lowassa iliyounganishwa na nguvu ya vyama vya upinzani?
(ii)
Jambo la pili ambalo CCM wanatakiwa wajiandae nalo baada ya “kumuengua”
Mheshimiwa Lowassa katika kukiwakilisha chama kwenye kugombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao, ni namna ya
kuishi na wana CCM ambao watakuwa ni “mamluki” wa Lowassa.
Na
kwa kuwa watakuwa hawajulikani, wanaweza “kuvuruga” mbinu zote za
ushindi za CCM na hatimaye CCM kushindwa au kushinda kwa ushindi
“mwembamba” mno ili wawaonyeshe Watanzania umuhimu wa Lowassa.
Je, CCM imejiandaa vipi kulikabili kundi la wafuasi wa Lowassa ambao wamo ndani ya CCM? Je, ni vipi wataweka mbele maslahi ya CCM kwanza wakati mgombea wao Lowassa hakupita?
Je, CCM imejiandaa vipi kulikabili kundi la wafuasi wa Lowassa ambao wamo ndani ya CCM? Je, ni vipi wataweka mbele maslahi ya CCM kwanza wakati mgombea wao Lowassa hakupita?
(iii)
Jambo la tatu ambalo CCM wanapaswa kujiandaa kukabiliana nalo baada ya
“kumkataa” Mheshimiwa Lowassa ni kitendo cha kunyimwa kura kwa mgombea
wa CCM au kitendo cha wafuasi wa Mheshimiwa Lowassa kupeleka kura zao
kwa mgombea wa Upinzani (hata kama atakuwa si Mheshimiwa Lowassa).
Wafuasi
wa Lowassa watachukua uamuzi huo wa hasira kwani hata ukiwasikia baadhi
yao hivi sasa, unaona wazi kwamba hawakujiandaa hata kidogo kushindwa
bali wamejiandaa kushinda kwa asilimia mia moja.
CCM
itapata wakati mgumu sana baada ya kumnyima Lowassa nafasi ya kugombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kwani Mheshimiwa
Lowassa ameshajijengea “mazingira” yanayoonyesha kwamba anapendwa sana
na idadi kubwa ya Watanzania wakiwemo baadhi ya Masheikh waliothubutu
kwenda kumuomba akubali kugombea cheo hicho cha urais.
Pia
baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo ambao wamekwenda kumuomba
agombee pamoja na kumfanyia “maombi” nyumbani kwake Dodoma. Wengine ni
baadhi ya waendesha “bodaboda” pamoja na wajasiriamali kadhaa.
Kwa
bahati mbaya sana, Mheshimiwa Lowassa bado hajawaambia wapenzi na
wafuasi wake kwamba ili kura ya mwendesha bodaboda au mamalishe au
kiongozi wa kidini iwe na thamani, ni lazima kwanza Kamati ya Maadili ya
CCM, Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu ya CCM na Mkutano Mkuu wa CCM;
wajiridhishe kwamba Mheshimiwa Lowassa “anauzika” na anaweza kuongoza
katika cheo hicho cha juu cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wa kumkubali Mheshimiwa Lowassa, CCM itambue kwamba siku itakapomtangaza Mheshimiwa Lowassa kuwa ndiye mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, ifahamike kwamba Wapinzani na Wafurukutwa wa siasa za upinzani wataitumia kadhia ya “Richmond” kama “uchafu” ambao unamnyima Mheshimiwa Lowassa sifa ya kuwa Rais safi wa kuiongoza Tanzania.
Hata kama wapenzi na wafuasi wa Lowassa wanasema kwamba ile ni ajali ya kisiasa na Mheshimiwa Lowassa hahusiki, hayo yatabakia kuwa ni maneno ya kitaalamu zaidi lakini kwa uoni wa kawaida wadhifa wa uwaziri mkuu umehusika kwa namna moja ama nyengine, na ndio maana aliridhia kujiuzulu na wala hakujenga hoja ya kubakia katika wadhifa huo ili afukuzwe na ithibitike kuwa kweli ameonewa.
Endapo CCM ikimpitisha Lowassa italazimika kuandaa utetezi mrefu, ni kwanini wasiitwe mafisadi?!!
Lakini jambo la pili ambalo CCM litawagharimu ni kitendo cha kumuadhibu Mheshimiwa Lowassa kwa adhabu ambayo wao wenyewe CCM wamejiridhisha kwamba ni kweli alivunja utaratibu kwa kuanza kampeni mapema.
Kitendo hicho kitawagharimu sana CCM baadaye katika kumnadi tena Mheshimiwa Lowassa na kusema kwamba ni mtu safi.

ujumla, CCM ina mtihani mgumu sana katika kazi ya kuchuja wagombea na
ni lazima ijiandae kwa faida na hasara kwa kila mgombea kutokana na
kumkataa au kumkubali kwao.
Lakini kwa kuanzia tathmini hiyo, waanze na huyu Mheshimiwa Lowassa. Je, CCM imejiandaa vyema na changamoto za kumkataa au kumkubali Lowassa? Kama haijajiandaa, inapaswa iamke kutoka katika “usingizi mzito” na ifanye tahtmini hiyo sasa.

Changamoto
ambazo CCM wanatakiwa kujiandaa nazo kwa kumkataa au kumkubali
Mheshimiwa Lowassa zipo nyingi sana, cha msingi ni kuwakumbusha wana CCM
kuwa makini kwani ni CCM pekee ndiyo inayoonekana kuwa kimbilio la
Watanzania kwa nafasi ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Baadhi
ya Watanzania huwa wanajaribu kubadilisha vyama katika ngazi ya
serikali za mitaa, udiwani na ubunge; lakini katika ngazi ya urais bado
wanaiamini CCM kuwaletea kiongozi bora.
Kwa muktadha huo, CCM nayo inalazimika kujipima na kutafakari mapema yote yanayotarajiwa kujiri katika Uchaguzi kwani uchaguzi sio tukio la ghafla bali ni tukio linalojulikana mapema hivyo mipango ipangwe mapema pia.