Wachezaji wa timu ya Umbrella Garden wakielekea katika lango kupiga mikwaju ya Penalti mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1
mchezaji wa Nyota Fc akipiga Penelti katika lango la Umbrela Garden
Naibu Meya wa jiji la Arusha Prosper Msofe akifurahia mashindano ya Ndondo Cup katika Viwanja vya Aicc Jijini Arusha.
.Mashabiki waliojitokeza Uwanjani hapo wakifuatilia meza kuu ambayo haipo Pichani
Mashabiki wa Nyota Fc wakishangilia Ushindi mara baada ya timu yao kuinyuka Umbrella garden magoli 6-5
Mlinda mlango wa timu ya Nyota Fc Hamis maarufu kama Dida akiwa anatizama mpira wavuni.
Ashura Mohamed-Arusha
Timu
ya Soka ya Nyota Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden
Fc kwa Magoli Sita kwa Matano na kufanikiwa kuondoka na kombe la
Ndondo Cup Sambamba na Kitita cha Shilingi Laki Tano Taslimu katika
fainali za Ndondo Cup zilizofanyika katika viwanja vya Aicc vilivyopo
Jijini Arusha.
Akizungumza
wakati wa fainali hizo Naibu meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe
alisema kuwa mashindano hayo ya ndondo Cup yamewakutananisha vijana
wengi ambao wamepata fursa ya kuonesha vipaji vyao.
Prosper
Msofe alisema kuwa mkoa wa Arusha una sifa nyingi lakini katika upande
wa Soka kwa sasa Hakuna timu ambayo ipo imara ambao inafanya vizuri
katika ligi mbali mbali hapa nchini.
Aidha
Msofe alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji zaidi na
kutengeneza timu moja ya mkoa Jiji la Arusha limepanga kununua eneo la
kiwanja nje ya mji na kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao
utawawezesha vijana wanaopenda kandanda mkoani Arusha kupata sehemu za
kuonesha vipaji vyao na badae kuchuja vijana 20 ambao wataunda timu moja
ambayo itawakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano mbalimbali hapa
nchini.
Kwa
sasa hatuna maeneo ya wazi na hili ni changamoto kwetu vijana wetu wana
vipaji lakini hawana sehemu ya konesha tumepanga kununua viwanja na
kuvitengeneza ili tuanzishe mashindano mbalimbali ambayo yatapelekea
tuapte timu bora itakayotuwakilisha vizuri mkoa wetu wa arusha alisema
Msofe
Kwa
upande wake waandaaji wa Ndondo Cup ambayo ni kampuni ya Tan
Communication Media wamiliki wa redio 5, Mathew Philip alisema kuwa
lengo la mashindano hayo ya ni kutoa burudani ya soka la Mchangani kwa
wakazi wa Jiji la Arusha lakini pia kuwapa vijana nafasi ya kuonesha
vipaji vyao katika mchezo wa soka.
Mathew
alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa burdani mbali mbali kwa
wakazi wa Jiji la Arusha huku akisema kuwa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu
hakukuwa na Soka la Mchangani ambalo lina vijana wengi ambao wana
vipaji na kuwawezesha kuonesha uwezo wao kwa kuwa sasa mpira ni Ajira.
Timu
zilizoshiriki ni Pamoja na Nyota Fc ambao waliibuka washindi,Ambrella
Garden ambao walishika nafasi ya Pili na kujinyakulia shilingi laki
tatu,F.F.U Oljoro Fc,Njiro Sports,Tanzanite Fc,Red Star Fc,Lemara Boys,