https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    VIJANA WA CHADEMA WAPO NJIANI WANAENDA BUTIAMA,SOMA KINACHOWAPELEKA HUKO



    Baadhi ya vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kutoka wilaya  za Nyamagana, Magu, Busega na Bunda wameanza matembezi ya siku sita  kuelekea katika kijiji cha Butiama kwenye kaburi la hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa  ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajia  kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.


    Matembezi haya ya vijana wa Chadema yameanzia eneo la igoma jijini Mwanza, mahali
    ambako mwaka 1967, Mwalimu Julius Kambarage 
    nyerere aliishia baada ya 
    kutembea kwa miguu kutoka mwitongo, Butiama mkoani Mara akiunga mkono 
    azimio la Arusha.


    Kiongozi wa msafara huo George Charles ambaye ni mwenyekiti wa baraza la vijana  wa Chadema (Bavicha) kata ya igoma anasema lengo la matembezi hayo ya 

    zaidi ya kilometa 260 pamoja na mambo mengine ni kupinga ufisadi, mauaji
    ya watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, vikundi vya kihalifu 
    vilivyoibuka jijini Dar es Salaam maarufu kama panya road, ambapo 
    wamelitaka jeshi la polisi kutowazuia na safari yao kwa vile matembezi 
    hayo ni ya amani kwa ajili ya kumuenzi baba wa taifa.

    Baadhi
    ya vijana wanaoshiriki matembezi hayo wanasema wameamua kufanya hivyo 
    kwa dhamira njema ili kuwahamasisha watanzania kujitokeza kujiandikisha 
    na pia kupinga uporaji wa raslimali za taifa unaodaiwa kufanywa na 
    baadhi ya watu wachache waliokabidhiwa dhamana ya uongozi na kusababisha
    ufa mkubwa kati ya wenye nacho na wasionacho huku wananchi walio wengi 
    wakiendelea kukabiliwa na umaskini.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: VIJANA WA CHADEMA WAPO NJIANI WANAENDA BUTIAMA,SOMA KINACHOWAPELEKA HUKO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top