Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
SERIKALI imeitaka
jamii kutumia vyandarua kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vyandarua
hivyo vitumike kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki.
Hayo
yamesemwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick wakati wa maadhimisho ya
siku ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka.
Sadick
amesema wafadhili mbalimbali wamekuwa wakiweka nguvu katika kupambana
na Malaria hivyo ni wajibu jamii kutumia Vyandarua hivyo kwa malengo
yaliyokusudiwa kwani kufanya hivyo kutaongeza uzalishaji wa uchumi
katika nchi kutokana na kuwa na afya iliyo bora.
Katika
maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo amezindua mpango wa ugawaji wa
Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na
wadau mbalilmbali kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Amesema
tangu kuanza kampeni hiyo ya kupambana na Malaria utafiti unaonyesha
Malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2012 na kufikia asiliamia 10
mwaka huu ambapo kupungua huko kumekwenda sambamba na kupungua kwa vifo
vya wajawazito pamoja na vifo vya watoto chini ya miaka mitano(5).
Sadick
amesema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara ya Kazi zinatakiwa
kuweka utaratibu kwa makampuni mbalimbali kupambana na Malaria na sio
kuwa sehemu ya hiari kwani kufanya hivyo kutaongeza ufanisi katika
makampuni pamoja na viwanda.
Wananchi
wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya siku
ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka, yaliyoanzia
katika viwanja vya Msasani na kuishia viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi
wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya siku
ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka, yaliyoanzia
katika viwanja vya Msasani na kuishia viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua katika maadhimisho ya siku ya Malaria
Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es
Salaam .
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akitoa hotuba yake katika
maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mtoto
Noel Peter akiwa amelala kwenye kitanda kilichowekwa Chandarua ikiwa ni
ishara ya kampeni ya kupambana na Malaria katika maadhimisho ya siku ya
Malaria duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi
wa Shirika la maendeleo ya Watu wa Marekani (USAID),Ana Bodibo–Memba
akizungumza leo na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Malaria
duniani katika viwanja vya Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa BG Tanzania,Stevenson Murray akizungumza leo na wananchi katika
maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika viwanja vya Msasani Jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Afya ya Ifakara ,Dk.Ladslaus Mnyone katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo hufanyika kila mwaka Aprili 25 yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Afya ya Ifakara ,Dk.Ladslaus Mnyone katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo hufanyika kila mwaka Aprili 25 yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.






