AZAM
FC imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani,
kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC jioni hii
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi
huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25,
nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.
Simba
SC ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na hata ikishinda mechi yake
ya mwisho itafikisha 47, hivyo kwa mwaka wa tatu mfululizo Wekundu wa
Msimbazi watakosa michuano ya Afrika.
Azam FC ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Brison Raphael, Frank Domayo, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche na Brian Majwega.
Azam FC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Saum Telela, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho.
Winga wa Azam FC, Brian Majwega akimtoka beki wa Yanga SC, Juma Abdul jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam |
Mrisho Ngassa wa Yanga SC akijaribu bila mafanikio kufunga langoni mwa Azam FC |
Beki wa Azam FC akimdhibiti winga wa Yanga SC, Andrey Coutinho |