https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Picha&Video:Kijana aliyebakiza inchi chache amfikie mtu mrefu zaidi duniani.


    Ikiwa rekodi ya mtu mrefu zaidi duniani inashikiliwa na Sultan Kosen raia wa Uturuki akiwa na urefu wa futi 8 na inchi2, huyu ni Broc Brown,(19) raia wa Michingan Marekani, mwenye urefu wa futi 7na inchi 8 na ametajwa kuwa kijana aliyebakiza inchi chache amfikie Sultan Kosen. Broc amebakiza  inchi 4 kumfikia Sultan ambaye yeye ana miaka 33.
    dorco
    Familia ya Broc iligundua utofauti wake baada ya kufikisha miaka mitano ambapo pia alianza shule akiwa na urefu wa mwanamke wa size ya kati. Mama yake anasema amekua akiongezeka inchi sita kila mwaka na kama ataendelea hivi basi yuko karibu sana kuvunja rekodi ya mtu mrefu zaidi duniani.
    dooooorc
    Hali hii imepelekea kuingia gharama ziada katika kumuhudumia kuanzia mavazi, chakula mpaka kitanda chake cha futi8  ambacho wazazi wake wanasema kiliwagharimu  zaidi ya $1000 kupata kitanda cha size yake pamoja na kiti chake spesho. Daktari amewaeleza kuwa hayo ni matatizo ya genetics (Gigatisim) (kuwa na maumbile makubwa ) na hakuna cha kufanya ili kumzuia Broc kuendelea kukua.
    Licha ya kuwa na Gigatisim, ugonjwa ambao humpata mtu mmoja kati 15,000 Broc ana matatizo ya kujifunza,  maumivu katika moyo, pamoja na uti wa mgongo ambapo pia hushindwa kutumia dawa za kupunguza maumivu kwani alizaliwa na figo moja tu.
    “Wanaume wengi wanaacha kukua wakiwa na miaka 22 na Broc ana miaka 18 sasa, mtu mrefu zaidi duniani ana futi8 na inchi 2 nadhani Broc anaweza kufika hapo akiendelea hivi na hakuna tutakachoweza kufanya kuzuia hilo” _Mama mzazi wa Broc.
    VIDEO FUPI IKIONYESHA SEHEMU KIDOGO YA MAISHA YAKE >>>
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Picha&Video:Kijana aliyebakiza inchi chache amfikie mtu mrefu zaidi duniani. Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top