Picha
ya aliyoitupia mapema leo asubuhi kupitia IG yake AuntyEzekiel ambayo
hadi sasa imeshapata LIKES nyingi pamoja na Comments huku watu
wakimuombea.
Huenda
ulipata kusikia habari za Staa wa filamu za kibongo, ‘Bongo Movie’ Aunt
Ezekiel ambaye kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram anatumia
IG Auntyezekiel, mapema asubuhi ya leo April 30, kupitia IG akaunti
hiyo ametupia picha ya tumbo lake. (Tazama picha hapo juu).
Hata
hivyo katika picha hiyo, Aunty Ezekiel aliandika: ‘Morning…’ ikiwa ni
sabahi kwa fans wake, ambaye hadi sasa ana fans walio m-follow 311K.
huku akiwa na wastani wa kila post yake anayotupia IG, kupata LIKES
nyingi zinazofikia zaidi ya 8,000 hadi 1,000.
Hata
hivyo, hadi Mtandao huu unarusha Exclusive hii tayari post hiyo
aliyoanika tumbo lake imeweza kufikisha LIKES zaidi ya 3,522 huku
akipata Comments zaidi ya 394.( Likes na Comments zinaongezeka hii ni
kwa muda tuliochukua taarifa).
Kama
ilivyo kawada ya mastaa wengi na watu maarufu kwa tabia ya kutojibu ama
kurejea kubadilishana mawazo na fans wao, ambao kwa post hiyo watu
wengi waliotembelea na kuchangia maoni yao wapo waliompongeza na
kumuombea huku wengine wakimponda na kumtukana kwa kuwaonyeshea kitumbo
hicho.
Wema akiwa na Aunty Ezekiel.
Modewji
blog iliweza kubaini kuwa kutokana na Aunty Ezekiel kuwa na ukaribu na
Wema Sepetu hali hiyo imefanya #teamDiamond kutembelea post hiyo na
kurusha maneno ya vijembe huku wengine wakimtukana na kumpa ‘makavu
Live’.
Baadhi
ya waliochangia akiwemo Magemmasi alimtupia dongo na kumuambia asimuige
Hamisa Mabeto ambaye ni model na aliwahi kupost picha kama hizo
kupitia mitandao ya kijamii na baada ya siku mbili alijifungua na
wengine wengi ambao maneno yao kwa maadili hatuwezi kupost hapa ila
unaruhusiwa kum-follow kupitia IG yake ya auntyezekiel na kuona hayo
yote.
Kimeeleweka:
Mtandao
huu kupitia vyanzo mbalimbali vya habari viliweza kuwasiliana na
wataalam wakiwemo madaktari ambao walieleza kuwa kwa kawaida mimba
kitaalamu huwezi ibashiria kitu hadi pale mama mjamzito anaposhikwa na
uchungu na kisha kupelekwa leba hivyo hata kama tumbo lipo kubwa kiasi
gani ama lipo dogo kiasi gani, kama ni mjamzito mwisho wa siku ni pale
anapojisikia uchungu ndipo atakapokimbizwa leba na kujifungua.
Alijibu
Daktari huyo wa Hospitali ya Kinondoni, hii ni baada ya kumhoji juu
ya athari anazoweza kuzipata mwanamke mjamzito pindi atakapokaa muda
mrefu na ujauzito licha ya kuwa tumbo lake la mimba kuwa kubwa.
Mimba
hiyo ya Aunt Ezekiel imekuwa ikifuatiliwa mara kwa mara na watu
mbalimbali huku wakitaka kuona anajifungua ambapo miezi kadhaa iliyopita
mitandao ya kijamii iliwahi kutoa taarifa za kujifungua kwa staa huyo
ambaye pia anamvuto wa asili na asiyechuja tokea kuingia kwenye soko la
filamu za kibongo.
Mose Iyobo katikati anayeelezwa kuwa ndiye ‘kidume aliyetundika mimba iyo’ kwa Aunty Ezekil (kulia), wa kusoto ni rafiki yao.
Hata
hivyo, kikubwa cha watu wengi wakiwemo fans wake kumsubiria ajifungue,
ni kuona mtoto huyo ni wa nani licha ya kuwa tayari Mose Iyobo ambaye
ni dancer wa Diamond Platnumz kubainika kuwa ndio baba kijacho wa
mtoto huyo wa staa.
Mbali
ya Iyobo pia wapo watu mbalimbali wanahusishwa wakiwemo watu maarufu
pia wanasiasa. Modewji Blog tunaweza kusema kimeeleweka kwani hii si
mara ya kwanza kwa staa huyo kuachia picha za tumbo lake, kwani kwa
upande wa model na video queen, ‘Master snake’ ama mwanadada hodari wa
kucheza na nyoka ambaye alipata umaarufu huo wakati wa ushiriki wake wa
mashindano ya Ulimbwende nchini, miaka ya nyuma, Hamisa Mabeto ambaye
naye licha ya kuficha kwa muda mrefu tumbo lake hilo, mwisho wa siku
aliweka wazi na baadae akatupia picha za ‘location’ akiwa amepiga picha
huku tumbo lake likiwa wazi, hata hivyo baada ya kuzagaa kwa picha
hizo, siku mbili tu akajifungua.
…Kimeeleweka kwa Aunty Ezekiel …tusubiri matokeo ambayo ni dakika 90, ingawa kuna dakika za nyongeza.