https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    TAARIFA KUTOKA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

    JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
    KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

    Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
    Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
    Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 15, May 2015
    Tele Fax : 2153426
    Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
    Tovuti : www.tpdf.mil.tz

    Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitishwa na taarifa za uvumi zilizotolewa kuenea kwenye mitandao ya kijamii face book, whatsapp na twitter zikieleza kuwa JWTZ inafanya usaili leo tarehe 15 May 2015 katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa wale waliosoma fani ya Computer science, IT, Electronics na Mechanical Enginering.

    JWTZ linapenda kuwajulisha wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo si za kweli ni uvumi, JWTZ lina utaratibu wake wa kuandikisha Jeshini ambapo hutoa taarifa katika vyombo vya habari kwa utaratibu ulio sahihi.

    Aidha, Jeshi linaendelea kusisitiza wananchi kuwa halina akaunti za mitandao hiyo na ni kinyume cha sheria kusambaza ujumbe kwa kutumia jina au nembo ya JWTZ watakao bainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.

                                                Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
                                                                 Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
                                                           S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TAARIFA KUTOKA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top