WAJUMBE
wa Sekreatrieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya (NEC)
ya CCM, jana walitembelea maeneno yaliyofikwa na mafuriko ya Mkoa wa
Mjini Magharibi kwa lengo la kuangalia na kuwafariji wananchi
walioathirika na mkasa huo.
Wakiongozwa
na Mwenyekiti wao, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Vuai Ali
Vuai, wajumbe hao wa Sekreatrieti walitembelea maeneo mbali mbali mkoani
humo ikiwemo Mpendae kwa Binti Amrani, Tomondo na Mwanakwerekwe, ambayo
yalikumbwa na kadhia hiyo.
Walitumia
nafasi hiyo kuwafariji baadhi ya wananchi waliathirika na mafuriko
hayo, ambapo baadhi nyumba zimejaa maji na nyengine kuanguka kuta zake,
na kusabababisha hasara kubwa.
Wajumbe
hao wamewataka wale wote waliokumbwa na janga hilo, kuwa na moyo wa
subra na kuiachia Serikali kupitia kitengo cha maafa kutafakari na kuona
nini la kufanya. Aidha, wametoa wito na haja kwa jamii nzima ya
Wazanzibari kuchukua tahadhari hasa wakati huu wa mvua za masika
zinazoendelea kunyesha.
Mvua
hiyo kubwa iliyonyesha kwa muda wa masaa matatu mfululizo, kuanzia saa
3:30, iliwafanya wananchi wa Manispaa ya Zanzibar na vVitongoji vyake
kushindwa kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.