Ronaldo amenukuliwa na gazeti
moja la michezo la nchini Ureno linalofahamika kwa jina la A Bola la
Jumamosi akisema kwamba, anafuraha kuwa kwenye klabu bora duniani,
anajipanga na anahakika msimu ujao utakuwa ni wa mafanikio.
“Nina furaha sana kuwa kwenye
klabu bora duniani, ninajipanga na ninaimani msimu ujao utakuwa ni wa
mafanikio”, aliliambia gazeti hilo.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno
amezungumza hadharani tangu alipowaambia waandishi wa habari kwamba,
hatozungumza kwenye vyombo vya habari hadi mwisho wa msimu baada ya timu
yake kupata kichapo kwenye mechi ya vilabu bingwa barani Ulaya kutoka
kwa Schalke 04 mwezi Machi.
Ronaldo kwa sasa yupo mapumzikoni
(likizo) Miami akila maisha baada ya pilika nyingi za msimu uliopita
kutokuwa na mafanikio kwa klabu ya Madrid.


0 comments:
Post a Comment