Baada
ya kushudia Neymar akifanya kitendo cha fujo kwenye mechi ya Copa
America, watu wengi walianzisha debate ya wachezaji watata uwanjani
kuwahi
kutokea kwenye historia ya soka. Hawa hapa ndio wanatajwa sana na wamepangwa kwa namba
10. Rene Higuita
Huyu ni kipa wa Colombia na ni maarufu sana kwa Scorpion Kick ambapo ali-save goli kwenye mechi dhidi ya England mwaka 1995.
Mwaka 1990 alijaribu kumpiga chenga Roger Milla na kupoteza mpira na Roger akacheka na nyavu. Huyu jamaa aliwai kukosa fainali za kombe la dunia mwaka 1994 baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumteka mtu
Mara nyingi alikua anahusishwa na muuza madawa maarufu Pablo Escober na aliingia kwenye vichwa vya habari kwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Pia aliwai kupimwa na kukutwa na matumizi makubwa ya cocaine mwilini mwake
9: Joey Barton
Midfielder wa Marseille ni mchezaji mwingine ambae ni mtata kupita kiasi. Aliwai kufungiwa mechi 12 kwasababu ya kushambulia mashabiki wa timu pinzani
Mwaka 2007 alihusishwa na ugomvi huko Liverpool city center na baada ya ugomvi huo alipelekwa jela miezi 6
8.Sinisa Mihajlovic
Huyu alikua ni kocha mtata kupita kiasi, aliwai kumfungia mchezaji asicheze tena chini yake baada ya kutokuimba wimbo wa taifa. Tatizo lake kubwa lilikua ni kugombana na wachezaji kwa vitu vidogo lakini reaction yake huwa inakua kubwa sana
7: Harald Schumacher
Anakumbukwa sana kwa kitendo alichokifanya kwenye mechi ya kombe la dunia 1982. Huyu jamaa kwenye nusu fainali ya kombe la dunia alimshambulia beki wa Ufaransa Battiston hadi kumvunja mbavu 3. Kitendo hicho kinakumbukwa hadi leo kwenye historia ya soka.
6.Luis Suarez
Huyu jamaa alipewa jina la ng’atang’ata kutokana na tabia yake ya kutia meno wachezaji wenzake uwanjani. Laiwaki kuwa na ugomvi na Evra, alitia meno Cheillini na wengine.
5.Edmundo
Jina lake ni Edmundo na aliwai kupewa jina la “Most hated player in Brazil”. Licha ya uwezo wake mkubwa uwanjani lakini alikua anashindwa kujizuia hisia zake na kujihusisha kwenye vurugu nyingi. Huyu jamaa aliwai kuwagonga watu wawili huko Rio De Janeiro akiwa amekunywa pombe lakini kesi yake iliishia juu kwa juu.
4.John Terry
Kuanzia kugombana na mapaparazi hadi kuhusishwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wa marafiki zake. John Terry aliwai kuhusishwa na kumtolea maneno ya ubaguzi beki Anton Ferdinand.
Pia aliwai kuhusishwa na fujo kwenye hotel ya Heathrow. Aliwai kufikishwa mahakamani kutokana na mambo ya fujo.
3. Eric Cantona
Maarufu sana kwa Kung-fu-kick attack kwa mashabiki wa Crystal Palace mwaka 1995 ambayo inaonekana kama ni doa kubwa sana kwenye maisha yake ya soka.
Kitu kingine aliwai kupiga mpira kwenda kwa mashabiki, kutoa jezi yake akitaka kuichana baada ya kufanyiwa sub na pia kumtolea maneno mabaya kocha Herni Michel.
2.Paolo Di Canio
Huyu jamaa alimaliza maisha yake ya soka kwenye club ya Milan kutokana na ubishani na fujo kati yake na kocha Fabio Capello. Pia alisepa Juve kwa kusababisha matatizo yale yale na kocha wake Giovanni Trapattoni
Pia huyu jamaa kichaa cha doggy aliwai kutia mtama refa baada ya kumlima kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Arsenal 1998. Hicho kitu kilisababisha kufungiwa mechi 11
1.Diego Maradona
Dawa za kulevya na huyu jamaa kuna ukaribu sana. Aliwai kurudishwa nyumbani baada ya mechi mbili tu baada ya kufeli kwenye test ya dawa za kulevya.
Uwanjani hadi nje ya uwanja Maradona ana matukio ya utata ambayo licha ya kuwa na uwezo wa kisoka ameshindwa kuwa mfano mzuri kwa vijana kwasababu ya maisha yake ya utata na matumizi ya dawa za kulevya