https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Hiki hapa alichokisema Hans Poppe baada ya maamuzi ya TFF kuhusu sakata la Messi

    hans-poppeBaada jana TFF kutoa maamuzi kuhusu utata uliojitokeza kwenye mkataba kati ya klabu ya Simba na Ramadhani Singano ‘Messi’, leo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe amesika kwenye kituo kimoja cha redio  cha jijini Dar es Salaam akizungumzia sakata hilo huku akihoji ni nani aliye mwambia Singano yupo huru?

    Poppe amesema kikao kilichofanyika jana na kuongozwa na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa hakikuwa na mamlaka wala madhumuni ya kuamua upi ni mkataba halali kati ya mkataba alionao Messi au mkataba uliopo Simba. Badala yake kilikuwa ni kikao cha kutafuta suluhu ili mambo yaweze kwenda sawa kati ya pande hizo mbili.
    “Kikao kilichofanyika jana hakikufanyika kwa madhumuni ya kuamua nani kashinda na nani kashindwa, hakikuwa na ‘mandate’ hayo, hakina maamuzi ya kusema mkataba huu ni halali na huu sio halali. Katibu mkuu wa TFF amesema wazi kilichofanyika jana ni ‘mediation’, pale hapakuwa na maamuzi ya kuchambua mkataba upi upo ‘right’ wala hawakufikia hatua hiyo”, amesema Poppe.
    “Ila walichokisema pale ni kwamba, kabla hatujafika kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ambako pale ni mashtaka sasa na hukumu, hivi hili suala halizungumziki? Ndio kitu kilichofanyika jana na kilitokana na yeye mwenyewe ‘Messi’ kuulizwa, wewe ulivyozua hili varangati Simba ulikuwa unataka nini, kuondoka  Simba? Akasema hapana mimi nataka kuendelea kuchezea Simba. Akaulizwa mwakilishi wetu Collins akasema mbona sisi na mkataba tumesha mpatia?”, aliongeza.
    “Ndio wakasema kama suala liko hivi linazungumzika, kwanini lisiende kwenye mkopndo huo. Kumbuka mwanzo mimi nilieleza kuwa, huyu mchezaji wakati amekuja kuhoji kuhusu mkataba wake na kuona kwamba yeye anazungumzia mkataba wake umeisha na sisi tunasema haujaisha, tulimweleza kwamba hili suala linazungumzika vizuri tu, kama wewe huutaki huu mkataba njoo tukae tukupe mkataba mpya lakini mkataba wako ni huu sasa yeye akaendelea kung’ang’ania na sisi tunaona hili suala ni bora lifike mwisho wake”, amesema.
    “Kama hatutaelewana hakuna mkataba mpya mezani tunarudi kwenye mkataba wetu ulipo kwamba sisi mkataba wetu unamalizika 2016, sasa ndio tutakwenda kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji hao ndio watakaotoa uamuzi sasa mkataba upi ni halali”, amefafanua.
    “Baada ya kutoka kwenye kikao cha jana, Messi kaenda kuzunmgumza kwamba yeye yuko huru sasahivi, aliyemwambia yuko huru nani? Mwesigwa kaulizwa pale kama mchezaji yupo huru kasema hapana, na haikutakiwa kuzungumza, mtu aliyetakiwa kuzungumza pale alikuwa ni katibu peke yake”, alisisitiza.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Hiki hapa alichokisema Hans Poppe baada ya maamuzi ya TFF kuhusu sakata la Messi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top