Viongozi wa klabu ya Yanga wakikabidhiwa mfano wa hundi ya zawadi ya bingwa wa ligi iliyomalizika yenye thamani ya shilingi miolioni 80 za Tanzania
Baba yake Simon Msuva (mzee Msuva) akiwa ameinua juu tuzo ya mfungaji bora wa ligi iliyokwenda kwa Simon Msuva, (kulia kwake) ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia na (kushoto kwake) ni mama yake Simon Msuva
Wazazi wa Simon Msuva wakiwa wameshika tuzo ya mtoto wao mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mh. Juma Nkamia aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo
Shabani Kado akipokea tuzo yake ya golikipa bora wa msimu uliomalizika
Mh. Juma Nkamia (kulia) akiteta jambo na Rais wa TFF Jamal Malinzi
Mwakilishi toka Mtibwa Sugar akipokea tuzo ya timu yenye nidhamu
Mbeya City nao walipata zawadi ya mshindi wa nne
Katibu mkuu wa Yanga Jonas Tiboroha (kulia) naye alikuwepo
Mh. Juma Nkamia akitoa hotuba
Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akiwa pamoja na baba yake Simon Msuva
Mke wa Juma Nkamia ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Viajana, Utamaduni na Michezo naye alikuwepo kwenye ugawaji wa tuzo (katikati) ni mtoto wa Naibu Waziri
Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm jana alimwagwa kwenye kinyang’anyiro cha kocha bora wa ligi msimu uliopita na tuzo hiyo kwenda kwa Mbwana Makata
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (kushoto) alikuwa ni mmoja kati ya waliokuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora
Hizi ndio tuzo zilizokuwa zinagombewa kabla hazijaanza kukabidhiwa kwa wahusika