Gari likiwa limebeba takataka katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Mabanda ya maonyesho ya sabasaba yakiendelea kufanyiwa kukarabati kwaajili ya maonyesho yatakayoanza Juni 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wazee wa kilimo kwanza wakiwa katika maandalizi ya maonyesho ya sabasaba.
Wanawake nao katika harakati za kuweka mazingira ya kupendeza katika mabanda ya maonyesho ya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
Mafundi wakitoa mizigo kwaajili maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Mwonekano wa nje katika viwanja vya sabasaba ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja hivyo.
HABARI NA PICHA NA EMMANUEL
MASSAKA,GLOBU YA JAMII.
HABARI NA PICHA NA EMMANUEL
MASSAKA,GLOBU YA JAMII.
ZIKIWA zimebaki siku 4 kufuguliwa kwa maonyesho ya Saba Saba hapa nchini, Makampuni 1500 toka ndani ya nchi na mengine 400 toka nje ya nchi yanatarajiwa kushiriki maonyesho hayo.
Akizungumza na Globu ya jamii leo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko ya Nje wa Tan Trade, Mrs Anna Florence Bulondo amesema katika maonyesho hayo, Banda la maonyesho la Wizara ya Elimu litakuwepo katika maonyesho hayo kwa mara ya kwanza.
Pia amesema nchi 25 toka sehemu mbalimbali duniani zinatarajiwa kushiriki maonyesho hayo.
Aidha amevitaja viingilio katika maonyesho hayo kuwa ni shilingi 3000 kwa watu wa wazima hiyo ikiwa Julai 1-6 huku akieleza kuwa siku ya kilele Julai 7 kiingilio kitakuwa shilingi 4000 kwa watu wazima na watoto wakiingia katika maonyesho hayo kwa shilingi 1000 mpaka mwisho wa maonyesho.