https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.

     
    Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera
    kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.
     OFISA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi Zanzibar.
    Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake kwa kusaidia Jamii.
    Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali wananchi wakati wa maafa  na kutowa shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
      WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya mvua hivi karibuni.
    Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya mvua hivi karibuni.

    MKUTANO WA TANO WA WADAU WA NSSF WAENDELEA LEO AICC, JIJINI ARUSHA

    Mwenyekiti wa Kikao cha kwanza siku ya leo katika Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika hilo, Magret Ikongo akiongoza kikao hicho leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
    Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akimpatia maelekezo, MC wa Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sauda Simba wakati wa Mkutano huo unaonedelea leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
    Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Kilimanjaro, Delfina Masika akitoa maelezo juu ya uendeshaji na muenendo wa Mfuko wa NSSF, wakati wa Mkutano wa tano wa Wadau NSSF unaoendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
    Mkurugenzi wa Mipango,Uwekezaji na Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yacoub Kidula akiwasilisha mada iliyohusu mambo ya Uwekezaji, kwenye Mkutano wa tano wa Wadau NSSF unaoendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

    Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la NSSF wakiwa kwenye Mkutano huo.
    Baadhi ya Watendaji wa Shirika la NSSF.



    Wadau wa Mkutano wa NSSF kutoka nchi za nje wakiwa kwenye Mkutano huo.


    Mkurugenzi wa Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii,  (SSRA), Lightness Mauki akitoa hoja kwenye Mkutano wa tano wa Wadau NSSF unaoendelea leo kwa siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

    Muwakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (RBA) YA nchini Kenya, Charles Machira akiwasilisha mada yake kwenye mkutano wa tano wa wadau wa NSSF, unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha leo.


    Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifatilia mkutano huo.
    Sehemu Wadau wa Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, wakifatilia mada mbali mbali.
    Wadau mbalimbali wakiuliza maswali katika kipindi cha maswali na majibu, kwenye mkutano wa tano wa wadau wa NSSF, katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC leo jijini Arusha.
    Balozi wa Mfuko wa NSSF, Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Mwasit Almas akifatilia mkutano huo.
    Muonekano wa Ukumbi wa AICC wakati wa Mkutano wa tano wa NSSF.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top