Utajisikiaje pale unapopewa chakula kwenye ndege alafu unakutana na kitu ambacho hukukitegemea?
Kuna hii ya abiri mmoja aliyekua anasafiri na ndege ya Air India kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Delhi kwenda London ambapo aliomba kupewa special order lakini baada ya kuletewa hakuamini alichokutana nacho ndani.
Baada ya muhudumu wa ndege kumletea Burger kama alivyoagiza abiria huyo hakuamini alipofunguia na kukutana na mjusi akiwa hai ndani kitendo ambacho hakikumkwaza yeye peke yake bali abiria wote ndani ya ndege hiyo na wote kuamua kususa kula chakula walichopewa.
Mara baada ya tukio hilo uongozi wa ndege hiyo uliomba radhi na kuahidi kutotokea tena lakini abiria wote walionekana kukasirishwa na tukio hilo.