https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    NYOTA WA CHILE ARTURO VIDAL APATA AJALI MBAYA, ALALA RUMANDE





    MWANASOKA Arturo Vidal anashikiliwa na Polisi wa Chile baada ya kupata ajali akiwa na gari lake aina ya Ferrari kwa madai alikuwa amelewa pombe.
    Nyota huyo wa Juventus na Chile, amesema kwamba hahusiki na ajali hiyo  ambayo imesababisha gari lake la kifahari lenye thamani ya Pauni 230,000 liwe 'nyang'a nyang'a' jana na mchezaji huyo alilala Polisi kabla ya kesi kupelekwa Mahakamani.
    Vidal ambaye anaongoza kwa mabao katika Copa America, hakuumia sana baada ya ajali hiyo, wakati mkewe Maria Teresa Matus pia naye hajaumia sana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa anatoka Casino na mekwe mchana.
    Arturo Vidal's red Ferrari after his car crash on a highway south of Santiago on Tuesday night
    Gari la Arturo Vidal, Ferrari nyekundu baada ya ajali kusini mwa Santiago jana usiku PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NYOTA WA CHILE ARTURO VIDAL APATA AJALI MBAYA, ALALA RUMANDE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top