Serikali ya Rwanda imelielezea tukio la kukamatwa mkuu wa usalama wa nchi hiyo Jenerali Karenzi Karake kuwa ni la kuchukiza mno.
Jenerali Karake, alikamatwa Jijini London kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow siku ya jumamosi, akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Kkimbari ya mwaka 1994.
Mkuu huyo wa usalama alikamatwa na maafisa wa polisi wa kufuatia kibali cha kukamatwa kilichotolewa na taifa la Hispania.